The House of Favourite Newspapers

Neymar Aenda Tena Barcelona

Mshambuliaji wa PSG, Neymar.

MSHAMBULIAJI wa PSG, Neymar juzi alitua kwenye timu yake ya zamani ya Barcelona na kukutana na wachezaji wenzake wa zamani.

 

Neymar alitua kwenye timu hiyo na kukutana na Luis Suarez na Rakitic ikiwa ni siku moja tangu alipoisaidia timu yake kupata ushindi dhidi ya Angers.

 

Wachezaji wa Barcelona waliokutana na Neymar walionekana kufurahia ambapo walikuwa wakizungumza muda mwingi huku wakiwa wanacheka.

Hii ni mara ya pili Neymar anakwenda Barcelona kuanzia alipoondoka hapo na kujiunga na PSG ya Ufaransa msimu uliopita.

 

Mchezaji huyo aliweka picha kwenye mitandao ya kijamii akiwa na wachezaji wenzake hao huku akiandika kuwa anafuraha sana kukutana nao.

Hata hivyo, baadhi ya picha alipiga huku akionyesha staili ya kushangilia ya mchezaji wa Manchester United, Jesse Lingard.

 

Inaaminika kuwa urafiki wa Neymar na Barcelona unaweza kufa mwishoni mwa msimu huu kama kweli Mbrazil huyo ataondoka na kwenda Real Madrid

Comments are closed.