Neymar Amshambulia Refa, Kisa Man United

Staa wa klabu ya Paris Saint – Germain na timu ya taifa ya Brazili, Neymar.

STAA wa Paris Saint Germain, Neymar ameelezea hisia zake za kuvurugwa na kitendo cha mwamuzi wa kati baada ya kuamuru ipigwe penalti ambayo iliwapa ushindi mnono Manchester United katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, usiku wa kuamkia jana.

 

Mwamuzi wa kati Damir Skomina aliwasiliana na wasimamizi wa huduma ya VAR dakika ya 90 baada ya beki wa United, Diogo Dalot kupiga shuti ambalo liligonga mkono wa beki wa PSG, Presnel Kimpembe na kuamuru ipigwe kona lakini baada ya kurudia tukio katika video akaamuru iwe penalti.

 

Neymar alikuwa karibu na eneo la uwanja muda wa tukio akijiandaa kuingia kushangilia lakini kibao kikageuka, baadaye alitumia ukurasa wake wa Instagram na kumshambulia Skomina kwa maamuzi yake pamoja na waamuzi wenzake.

 

“Hii ni aibu, wanaruhusu watu wanne ambao hawajui soka kurudia tukio, angetoaje mkono wake wakati ulikuwa nyuma, huu ni upuuzi,” aliandika Neymar

Toa comment