The House of Favourite Newspapers

Neymar atoa hatma yake PSG, Tutabeba UEFA

0

Kiungo mshambuliaji wa klavu ya PSG, Neymar amesema kwasasa anafanya mazungumzo na klabu yake hiyo na kusisitiza kuwa anajisikia vizuri na mwenye furaha tele.

 

Neymar ameyasema hayo wakati akiwa anazungumza na wanahabari kuhusu maandalizi ya mchezo wa kesho Aprili 28, 2021 wa nusu fainali ya kwanza wa ligi ya mabingwa barani Ulaya 4:00 usiku dhidi ya klabu yake ya PSG na Manchester City kwenye uwanja wa Pac de prince nchini Ufaransa.

 

Neymar amesema.“Nimekwisha liongelea hili mchezo uliopita, nina furaha sana hapa Paris. Ninafanya mazungumzo na PSG, nina jisikia vizuri na nina furaha”.

 

Katika kuzungumzia jinsi mchezo huo utakavyokuwa na malengo ya PSG msimu huu, Neymar amesema:

 

“Utakuwa ni mchezo mgumu, Manchester City ni timu kubwa na PSG ni miongoni mwa timu kubwa Duniani. Mwaka uliopita tulifika fainali, mwaka huu tun aimani tutashinda kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya”.

 

“Tunapaswa kuendelea kucheza kwa juhudi na kucheza vizuri kama kweli tunataka kubeba kombe ambalo tunalitaka kwa hudin auvumba.”

 

Mara ya mwisho PSG kukutana na Manchester City, PSG ilitolewa kwenye hatua ya robo fainali miaka mitano iliyopita.

Leave A Reply