Neymar Aumia Tena Kifundo cha Mguu, Kuikosa Copa America
NAHODHA wa Timu ya Taifa ya Brazil na Klabu ya PSG, Neymar Jr ameumia tena kifundo cha mguu timu yak ikicheza na Qatar katika Uwanja wa Estadio Nacional hivyo atakosekana katika michuano ya Copa America.
Hili ni pigo lingine katika maisha ya soka ya Neymar kwa kipindi cha miaka miwili tangu alipoumia mwaka jana wakati wa michuano Klabu Bingwa Barani Ulaya (UEFA) na kumwka nje kwa mizi kadhaa hadi Fainali za Kombe la Dunia ndipo akaingia tna uwanjani.

Ameanza kusumbuliwa na majeraha mara kwa mara, Wengine wanatabiri ndio ukingo wa utawala wake kama ilivyokuwa kwa wabrazil waliomtangulia (Robinho na De Lima, Pato n.k) ambao soka lao lilikumbwa na maswahibu ya majeraha ya mara kwa mara.
Mpira una maajabu yake wakati mwingine, huu ni muda wa mwanadamu mwingine msumbufu kutawala dunia. Yawezekana ni Richarlson au mwingine kuvaa viatu vya Neymar.


Comments are closed.