NEYMAR AVULIWA UNAHODHA BRAZIL

NEYMAR amevuliwa unahodha wa timu ya taifa ya Brazil kufuatia kutoelewana na kocha wake, Tite. Staa huyo wa PSG, alikuwa ndio anatazamiwa kuwa nahodha wa Brazil kwenye michuano ya Copa America inayoanza Juni 14 hadi Julai 7, mwaka huu.

 

Neymar inasemekana amevuliwa unahodha kutokana na matatizo ya utovu wa nidhamu kwenye kambi ya timu hiyo. Tite amemteua Dani Alves kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Brazil wakati wa michuano hiyo.

 

Alves, 36 anatazamiwa kuiongoza Brazil wakati wa mechi za kirafiki dhidi ya Qatar na Honduras hivi karibuni.

 

Neymar amekuwa na matatizo ya utovu wa nidhami kwani hivi karibuni alimpiga ngumi shabiki baada ya timu yake ya PSG kufungwa kwenye mechi ya fainali ya Coupe de France.

Loading...

Toa comment