The House of Favourite Newspapers

Neymar Coutinho Bonge la Dili Barcelona

Na Mwandishi Wetu/ CHAMPIONI/GPL

KIUNGO mshambuliaji wa Barcelona, Neymar amedai kama kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho atatua Camp Nou litakuwa ni bonge la dili kwani supastaa huyo wa Liver ameiva kuichezea Barca.
Kumekuwa na tetesi za mara kwa mara kuwa Coutinho anaweza kujiunga na Barcelona lakini zimekuwa zikikanushwa vikali na uongozi wa timu yake.
Coutinho amefanikiwa kufunga mabao 35 kwenye michezo 170, aliyoitumikia Liverpool kuanzia alipojiunga nao akitokea Inter Milan mwaka 2013.


Neymar, ambaye ni rafiki mkubwa wa Coutinho walikutana pamoja kwenye timu ya taifa ya Brazil na ndipo aliposema kuwa kiungo huyo anaweza kuwa sahihi kwenye timu hiyo.
Barcelona imekuwa ikitamba ikiwa na wachezaji mahiri duniani Lionel Messi na Luis Suarez pamoja na Neymar na inaonekana kuwa Coutinho anaweza kuungana nao.
“Mchezaji wa Ligi Kuu England ambaye natamani acheze Barcelona ni Coutinho. Naamini huyu ndiye mchezaji anayeweza kufiti kwenye kikosi cha Barcelona, ni mchezaji mahiri sana,” alisema Neymar, nahodha wa Brazil.
Kwa msimu huu Coutinho ameshafunga mabao sita wakati timu hiyo chini ya kocha  Jurgen Klopp, ikipambana kumaliza kwenye nafasi nne za juu.

Comments are closed.