The House of Favourite Newspapers

Neymar Kubaki Barcelona kwa Miaka 5

0

NeymarNeymar.Neymar 2Neymar na SuarezNeymar na MessiNeymar na Messi

KAPTENI wa Timu ya Taifa ya Brazil anayekipiga kunako Klabu ya Barcelona ya Hispania, Neymar Dos Santos mwenye umri wa miaka 24 ameweka wazi kuwa ataendelea kubaki klabuni hapo kwa miaka mingine mitano ijayo.

Neymar aliyekuwa akihusishwa kujiunga na Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) kwa dili kubwa zaidi amesema kuwa anapenda kuendelea kuichezea Barca na hiyo ndiyo imekuwa ndoto yake ya miaka yote kuwatumikia magwiji wa Catalan.

Rais wa Barcelona, Josep Bartomeu  amesema Neymar amekubali dili jipya la kubaki klabuni hapo na atakamilisha taratibu za kusaini siku za usoni huku akiongeza kuwa watamchukua pia Samuel Umtiti wa Lyon kwa paun euro milioni 20.

Neymar alijiunga na Barca mwaka 2013 akitokea klabu ya Santos ya Brazil na ameisaidia Barca kunyakuwa ubingwa mara kadhaa ambapo msimu uliyoisha Mei, Barcelona ilinyakuwa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania (LaLiga) 2016/17.

REKODI YA NEYMAR

2009-13: Santos – Games 225 Goals 136

2013-: Barcelona – Games 141 Goals 85

……………………………………………………………….

Total

Games: 366

Goals: 221

Leave A Reply