The House of Favourite Newspapers

Neymar Kuumia, Mtoto wa George Weah Aitwa Kikosi cha Kwanza PSG

 

IKIWA ni saa chache baada ya mshambuliaji wa PSG ya Ufaransa na Timu ya Taifa ya Brazil, Neymar kupelekwa nchini kwao kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji, chipukizi wa PSG, Timothy Weah ambaye ni mtoto wa nyota wa zamani wa klabu hiyo na Rais wa Liberia, George Weah amejumuishwa kwenye kikosi cha kwanza.

 

 

Kocha Emery Unai amemtaja Timothy (18) kwenye kikosi cha wachezaji 18 watakaosafiri leo kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Ufaransa dhidi ya Troyes.

PSG inakabiliwa na mapungufu katika safu yake ya ushambuliaji baada ya kuumia kwa Neymar, huku Kylian Mbappe na Edinson Cavani wakipumzishwa kwenye mchezo wa leo.

 

 

PSG ina kibarua kigumu mbele ya mahasimu wao Real Madrid baada ya kupigwa bao 3-1 katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.  Timothy hunenda akapangwa kwenye mechi ya marejeano na dhidi ya Real Madrid, Jumatano ya Machi 7 iwapo atafanya katika mechi hii ya Troyes.

 

Timothy anajaribu kutembelea nyota ya baba yake ambaye aliwahi kuichezea PSG kwa miaka mitatu na kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia mwaka 1995 kabla ya kuhamia AC Milan.

Comments are closed.