NGASA AOMBA NAMBA STARS

WINGA wa Yanga, Mrisho Ngasa amesema kuwa anahitaji kurudi kwenye timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuendeleza rekodi yake ya ufungaji bora wa muda wote.

 

Ngasa alikuwa shujaa kwenye mchezo wa juzi, dhidi ya Azam FC baada ya kufunga bao moja nala pekee kwa Yanga, kwenye mtanange uliopigwa katika Dimba la Uhuru, Dar.

 

Ngasa anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Taifa Stars, akiwa amefunga jumla ya mabao 25 toka alivyoanza kuitwa kwenye kikosi hicho katikati ya miaka ya 2000.

 

Akizungumza Spoti Xtra, Ngasa alisema kuwa bado anahitaji na anatamani kurudi katika kikosi cha timu ya Taifa kwa kuwa anahitaji kuendeleza rekodi yake ya ufungaji bora wa muda wote.

 

“Natamani kurudi kuitumikia Taifa Stars, ili niendeleze rekodi yangu ya ufungaji bora wa muda wote, kwa kuwa mimi ndiye ninayeshilia rekodi hiyo hadi sasa,” alimaliza Ngasa.

Na: ISSA LIPONDA, 

Toa comment