The House of Favourite Newspapers

Ngoma akicheza na Busungu ni mabao tu

0

KWA moyo mweupe kabisa, straika wa Yanga, Donald Ngoma, amesema anajisikia furaha kucheza pamoja na Malimi Busungu kwani upambanaji wake unampa nafasi ya kufunga mabao kirahisi.

Kauli hiyo ya Ngoma imekuja siku chache baada ya wawili hao kila mmoja kuifungia Yanga bao moja na kuiwezesha timu yao kuifunga Mtibwa Sugar mabao 2-0 katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Ngoma alisema: “Busungu ni mchezaji mzuri ambaye muda mwingi anapambana, sasa usumbufu wake kwa mabeki unaifanya timu ishambulie muda wote.

“Wakati yeye akileta usumbufu sisi huku tunatengeneza nafasi nyingi za kufunga na kama akiendelea kupangwa pamoja na mimi basi naamini nitafunga sana msimu huu.”

Wakati Ngoma akiwa na mabao manne katika ligi kuu ambayo ni sawa na straika mwingine wa Yanga, Amissi Tambwe, Busungu yeye amefunga mawili.

Leave A Reply