Ngoma Atupwa Nje Yanga Dhidi ya Kagera Sugar

Mshambuliaji wa ki­mataifa wa Yanga, Donald Ngoma (kushoto) akifanya yake.

 

MSHAMBULIAJI wa ki­mataifa wa Yanga, Donald Ngoma, raia wa Zimba­bwe amepewa wiki moja ya mapumziko huku akiwa chini ya uangalizi wa daktari kufuatia ku­sumbuliwa na nyama za paja hivyo kuna asilimia kubwa ya kukosa mchezo dhidi ya Kagera Sugar Jumamosi.

 

Ngoma alianza kuumwa nyama za paja hivi karibuni ambapo amelazimika kupewa siku saba kwa ajili ya mapumziko ili kuangalia afya yake kabla ya kuanza mazoezi mepesi.

Donald Ngoma mwenye jezi namba 11.

Akizungumza na Champi­oni Jumatano, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema, Ngoma amepewa siku saba za mapumziko kwa ajili ya kuangalia afya yake huku akiwa anaendelea na matibabu ili kuimarika kwa ajili ya kurejea akiwa salama kwa ajili ya mapambano ya ligi.

 

“Ngoma amepewa siku saba za mapumziko kwa ajili ya kuangalia afya yake kutokana na tatizo lake la nyama za paja zinazomsum­bua akiwa chini ya uangalizi wa daktari ambapo amepewa muda huo tangu juzi.

 

“Baada ya kumaliza siku hizo ndipo atalazimika kuanza mazoezi mepesi ya kumjenga, lakini kwa upande wa wache­zaji wengine wapo vizuri wanaendelea na programu kama kawaida,” alisema Ten.

 

Yanga inacheza Jumamosi ijayo na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera.

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment