The House of Favourite Newspapers

Ngoma, Chirwa Wapangwa Kuimaliza Simba

AZAM FC imesema haina hofu na mchezo wao wa ligi dhidi ya Simba utakaopigwa Oktoba 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru kutokana na kuanza kutengemaa kwa safu yao ya ushambuliaji inayoongozwa na Donald Ngoma na Obrey Chirwa.

 

Ngoma kwa sasa ndani ya ligi ametupia mabao mawili msimu huu jambo ambalo limefufua matumaini kwa benchi la ufundi na wachezaji kuamini kwamba atarejea kwenye ubora wake na kutimiza majukumu kwenye michezo yao yote ya ligi.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche alisema kuwa ana imani na kikosi chake kutokana na kasi ambayo wameanza nayo jambo linalowapa matumaini kupata ushindi mbele ya Simba.

 

“Tatizo kubwa lilikuwa kwenye ushambuliaji kwani nafasi tunatengeneza nyingi, hilo tumelifanyia kazi na kwa sasa taratibu linamalizika mpaka kufika siku ya mchezo dhidi ya Simba tutakuwa tumepata kitu kipya.

 

“Malengo yetu ni kuona tunapata ushindi na safu ya ushambuliaji ule ubutu wake umeanza kumeguka ndiyo maana tunaona hata Ngoma naye amefunga hata kwenye mechi zetu za kirafiki bado anaonyesha kile ambacho tunakihitaji, washambuliaji wetu wote ikiwa ni pamoja na Chirwa wanaongeza ari ya timu kupambana,” alisema Cheche.

MLYUKa, Dar

Comments are closed.