The House of Favourite Newspapers

Ngoma Kutua Singida United, Tafadzwa Kutinyu Yanga

0
Mshambuliaji wa Yanga, Mzimbabwe, Donald Ngoma.

LEO Jumatano ya Novemba 15, 2017, dirisha dogo la usajili limefunguliwa ambapo litazihusu timu za Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili. Wakati dirisha hilo likifunguliwa leo, mapema tu timu 16 za Ligi Kuu Bara zimeanza mawindo zikisaka wachezaji kwa ajili ya kuimarisha vikosi vyao.

Miongoni mwa timu hizo ni Simba, Yanga, Azam Singida United.

Timu hizo zimekuwa zikisaka saini za wachezaji kadhaa kutoka timu tofautitofauti, huku zingine zikitaka kuchukuliana wachezaji wenyewe kwa wenyewe ambapo mpaka usajili huo unamalizika, sura hizi zinaweza zisionekane kwenye timu zao za sasa.

Mshambuliaji wa Yanga, Mzimbabwe, Donald Ngoma, anatajwa kuhitajika na Singida United, ili wao wamuachie Mzimbabwe, Tafadzwa Kutinyu anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji.

 

Lakini pia, Amissi Tambwe wa Yanga, naye kwa mbali anatajwa kutakiwa kuondoka ndani ya timu hiyo kutokana na kile kilichoonekana msimu huu hana msaada baada ya kushindwa kucheza hata mechi moja kutokana na kusumbuliwa na goti. Yanga pia inataka saini ya kiungo wa Mtibwa Sugar, Mohammed Issa ‘Banka’ ambaye katika mechi dhidi yao msimu huu pamoja na ile na Simba, aliwavuruga vigogo hao na kuanza kummezea mate.

Kwa upande wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo huenda akatolewa kwa mkopo au akauzwa kabisa baada ya kutokuwa na nafasi ya uhakika ndani ya kikosi hicho ambapo kwenye mkataba wake umebaki
takribani miezi sita. Wachezaji wengine ambao wanaweza kuzihama timu zao ni Said Ndemla, Juma Liuzio na Mohammed Ibrahim ambao wote ni wa Simba, pamoja na Anthony Matheo wa Yanga.
kikosi hicho ambapo kwenye mkataba wake umebaki
pamoja na Anthony Matheo wa Yanga.

Leave A Reply