The House of Favourite Newspapers

Ngoma: Nimepona Sasa, Subirini Mabao!

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Donald Ngoma, raia wa Zimbabwe ambaye alikuwa nje kwa zaidi ya miezi 10, ameibuka na kuweka wazi kuwa sasa amepona kikamilifu na yupo tayari kwa ajili ya mapambano huku akiwaahidi mambo mazuri uongozi wa timu yake ya Azam.

 

Ngoma aliyetua Azam FC akitokea Yanga SC, juzi Ijumaa alirejea tena uwanjani kwa mara ya kwanza baada ya kuwa nje kutokana na matatizo ya goti yaliyokuwa yanamsumbua.

 

Mzimbabwe huyo alicheza pambano lake la kwanza la ligi baada ya kupita kwa muda huo dhidi ya Lipuli FC lililopigwa Uwanja wa Azam Complex jijini Dar na kumalizika kwa suluhu.

 

Nyota huyo aliyetua Bongo akitokea FC Platinum ya Zimbabwe, amesema kwa sasa yupo kamili kwa ajili ya purukushani za ligi baada ya kupona majeraha hayo ambapo jukumu lake lililopo mbele ni kuibeba Azam kwenye mechi zake.

 

“Nashukuru kwamba nimepona na nimerejea tena uwanjani, ninawashukuru uongozi wa timu yangu ya Azam kwa kila kitu.

“Baada ya kurejea kwa sasa kazi ni moja pekee ya kuisaidia timu kupata matokeo mazuri na pointi kwenye michezo yetu. Mechi na Lipuli FC tumejitahidi kutafuta matokeo lakini imeshindikana.

“Niwaambie tu mashabiki kwamba wasubiri mambo mazuri kwani nimerejea tena kwa mara nyingine,” alisema Mzimbabwe huyo baada ya suluhu ya Azam dhidi ya Lipuli.

Said Ally, Dar es Salaam

UCHAWI!! MANARA Amlipua Ajibu Imani za Kishirikina

Comments are closed.