The House of Favourite Newspapers

NGUMI ZA GLOBAL TV: IDD PIALALI Vs REGI CHAMPION (Marudio)

0


Pambano ya Idd Pialali dhidi ya Regin Champion kutoka DRC lilikuwa gumzo kubwa kutokana na mashabiki kuwashangilia muda wote kufuatia mtindo walioamua kuutumia wote.

Ipo hivi, kabla ya mabondia hao kupanda ulingoni walitambiana vya kutosha, Pialali aliahidi kumuua mpinzani wake na Champion alisema kwamba mpinzani hautomaliza raundi tatu sasa kilichokuja kutokea acha kabisa.

Katika raundi ya kwanza mabondia walionyesha ushindani mkali kwa kutumia dakika moja kwa kupigana mfululizo ngumi za uhakika kabla ya kila mmoja kusogea nyuma na kuanza kutupa makonde ya kwambali hali iliwafanya washangiliwe muda wote.

Licha ya hivyo mvuto wao uliongezeka kwa kuwa k mabondia wote kuwa na ‘footwork’ ya uhakika licha ya kuteswa na ulingo ambao muda mwingi ulionekana kuteleza kwa ngumi zao zilitumia akili ufundi mkubwa.

Pialali aliweza kumudu vyema raundi zaidi ya saba kutokana na kuchanga staili tofauti ili kumpa ugumu mpinzani wake ambaye alikuwa mbishi kutokana na kutaka kulazimisha kupiga KO akaitumia vyema Pialali kuweza kupiga ngumi za pointi zilimuwezesha kuubakisha ubingwa GlobaTV, Afrika Mashariki na Kati.

Leave A Reply