Ngwair: Bado Nalia tu na Tanzania
ALBERT Keneth Mangwair a.k.a Mimi, a.k.a Ngwair, alizaliwa Novemba 16 1982. Mei 28, 2013 msanii huyo akajitenga na dunia hii na kuuacha muziki wa Hip Hop, Bongo ukiwa njia panda.
Wapo wanaosema kwa Bongo hakuna msanii anayefikia kipaji alichokuwa nacho Ngwair, ukikubali, ukikataa, toa hoja.
Leo nimeona nikuletee salamu kutoka kwa msanii huyo ambaye amelala kaburi kwa zaidi ya miaka minane sasa. Salamu hizo nitazitoa kwenye mashairi ya wimbo wake uitwao Masikini Mwenzangu aliotoa mwaka 2013.
“Baada ya m weka z usikie kizungu zungu jinsi ukoloni unafanya mambo mpaka leo, kuongoza jamii sio kumtawala mkeo, najiuliza maisha yangekuwaje bila mziki, hivi mtaani ingekuwa vp?”
Unapochezea muziki, ujue unacheza na kitu kikubwa sana dunia. Salamu za Ngwair toka kuzimu zinakuuliza dunia ingekuwaje bila muziki?
Hakuna disko, hakuna kwaya, hakuna kinanda, hakuna sauti zozote za kuburudisa, mwanzo mwisho fulu kuzungumza; mtaani kungekuwaje?
Bila shaka hizi ni hisia za mbali za msanii huyo. Hebu fikiria akiwa kuzimu halafu unasikia wimbo wake wa Masikini Mwenzangu wenye mashairi haya unapigwa utahisi nini?
“Bado nalia tu na Tanzania yangu/kweli mali ni nyingi wale wachache wenzangu/me nalia na masikini wenzangu/eeh baba Mungu sikia kilio changu/issue is harder tuna suffer/sikia kilio changu/issue is harder tuna suffer/me nalia like…”
viongozi wa siasa kama viongozi wa dini,
mengi wanaongea coz silaha yao ni ulimi,
Mh.spika Tanzania huru inazidi zeeka tayari ni miaka 50,
mengi mmetuahidi pia ahadi ni deni…
Ngwair kalala na hivi karibuni itakuwa ndiyo bethdai yake lakini bado analia na nchi yake, ‘Rest In Peace’ mwana Hip Hop makini; si vibaya na wewe msomaji ukaitikia Amina ili maisha yaendelee.
@manyota_rich-0714 895 555