Meneja wa Kanda wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Injinia Nyirabu Musira akimkabidhi Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio mchoro wa jinsi jengo la Makao Makuu ya Ewura Dodoma litakavyokuwa.
Meneja wa Kanda wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Injinia Nyirabu Musira leo amemkimkabidhi Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio mchoro wa jinsi jengo la Makao Makuu ya Ewura Dodoma litakavyokuwa.
Makabidhiano hayo ya Ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya Mamlaka hiyo yamefanyika jijini Dodoma.
Shirika la Nyumba limepewa kandarasi ya kujenga jengo hilo lenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 10 ambalo litakuwa makao makuu ya Mamlaka hiyo nchini. NHC imepewa dhamana ya kuusanifu, kujenga na kuusimamia mradi huo.
Comments are closed.