The House of Favourite Newspapers

PSPF wazindua mpango wa matibabu kwa wanachama wa mfuko huo

0
saini

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, SSRA, Omar Kahlfan, (atikati), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Neema Muro, (wapili kushoto), Meenja wa Mpango wa Uchagiaji wa Hiari wa PSPF,Mwanjaa Sembe, (wakwanza kushoto) na maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF (kulia walosimama), wakishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayinhu, (kushoto) na Kaimu MkurugeNzi Mkuu wa NHIF, Michael Mhando, wakitia saini .

Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Michael Mhando, (wapili kulia), wakizindua mpango huo huku Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Omar Khalfan akishuhudia
Bw. Mayingu, (kushoto) na Bw. Mhando wakibadilishana hati baada ya kuzisaini.
 Bw. Mayingu akitoa hotuba yake.
 Bw. Mhando akitoa hotuba yake.
Maafisa kutoka NHIF
Mwanachama wa PSPF, akisoma vipeperushi, vyenye maelezo na huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo.
Mmoja wa waandishi wa habari akijaza fomu za kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari PSS
 Kaimu Murugenzi Mtendajiw a NHIF, Bw. Michael Mhando (kushoto), akifurahia jambo na Meneja Uendeshaji wa PSPF, Bi. Neema Muro
Mwanachama wa mpango wa Uchagiaji wa Hiari PSS, akipokea kadi ya bima ya Afya, kutoka kwa mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Omra Khalfan (kulia)
Mwanachama wa SPF, Constantine Edward (kushoto) akipokea kadi yake.
 Meneja Msoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Costantina Martin,akitoa maelezowakati wa hafla hiyo
Meneja wa Mpango wa Uchangiajiwa Hiari, PSS, wa Mfuko wa Penshni wa PSPF, Bi.Mwanjaa Sembe, (wakwanza kulia), na afisa wa PSPF, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafaidika wakwanza wa mpango wa Mfuko huo kuwapatia matibabu wanachma wake wa mpango wa PSS
Mzee Mohammed Madenge, watatu kushoto), ambaye ni Mwanachama wa PSPF, wakwanza kufaidika na mpango wa bima ya afya, akitoa neon la shkrani kwa niaba ya wenzake.
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, wameingia makubaliano yatakayowezesha wanachama wa PSPF, kupitia mpango wa Uchangiaji wa Hiari yaani PSS, kuanza kupata matibabu kwenye hospitali zote zenye mkataba na NHIF.
Makubaliano hayo yametiwa saini leo Jumatano Novemba 18, 2015, kati ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw.Michael C.t.M Mhando na kufuatiwa na uzinduzi rasmi ambapo wanachama wa kwanza zaidi ya 10 wamepatiwa kadi za Bima ya Afya.
Hafla hiyo ilifanyika makuu ya PSPF, jingo la Jubilee Towers jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Mayingu alisema, uamuzi huo wa PSPF kushirikiana na NHIF, ni utekelezaji wa malengo na ahadiz a serikali ya awamu ya tano chini ya Rais, Dtk. John Pombe Magufuli, ambaye aliwaahidi Watanzania wote wanapata huduma za afya zilzio bora.
“ Katika kuhakikisha ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais inatimizwa PSPF kwakushirikiana na wenzetu wa Mfuko waTaifa wa Bima ya Afya tutatoa huduma za afya kwa wanachama wa Mpango wa Uchangaji wa Hiari wa PSPF.” Alsiema Bw. Mayingu katika hotuba yake.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Michael Mhando alisema, wakati PSPF wamebobea katika suala la pesheni, NHIF wao wamebobea katika kutoa huduma za afya, hivyo ushirikiano wa Taasisi hizi mbili zenye uzoefu wa kuhudumia maisha ya Watanzania, utakuwa umewapa unafuu mkubwa wa maisha. wajasiriamali wadogo ambao kwa kuwekeza katika afya kutawawezesha ushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla

 

Leave A Reply