Ni Balaa! Cheki Jamaa Alivyoondoka na Milioni 20 Kimasihara
Mshindi wa nne wa droo kubwa ya kampeni ya Vodacom Tanzania Plc ‘Ni Balaa, Kila Mtu ni Mshindi’ George Thobias (Kushoto), akipokea mfano wa hundi ya shilingi million ishirini kutoka kwa Meneja Mauzo Mwandamizi Kanda ya Ziwa wa Kampuni hiyo, Victoria Ngoya (kulia), katika Duka la Vodacom lililopo Jijini Mwanza mwishoni mwa wiki iliyopita. George pia amepata nafasi ya kuchagua shule anayotaka na kisha Vodacom wataenda kukarabati maktaba ya shule hiyo.