Ni Balaa! Wateja wa Vodacom Waendelea Kushinda, Mmoja Ashinda Hadi Shilingi Milioni 20
Arusha: Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania (PLC) imetoa zawadi kwa washindi wa kampeni mpya ya ni Balaa kila mtu ni mshindi, ikiwemo mshindi mkuu tsh 20,000,000 na tsh 500,000 kwa washindi watano baada ya kushinda kwenye droo ya kampeni hiyo kwa mikoa ya Kaskazini.
Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa Vodacom, George Venant, amekabidhi zawadi kwa mshindi mkuu Bankason Yusuph, kiasi cha tsh milioni 20,000,000 Mkoani arusha, akiwa ni mshindi wa zawadi kuu wa kwanza kupatikana kwenye kampeni hiyo mpya ya ni Balaa kila mtu ni Mshindi, wakifuatiwa na shindi wengine ambayo imeanza rasmi Agosti nne mwaka huu.
George amesema kampeni hiyo ina lengo la kunufaisha wateja na jamii kwa ujumla na kuhakikisha kila mshiriki anapata nafasi ya kushinda zawadi za kila siku, wiki na mwezi, pamoja na washindi watano wa zawadi kuu.
Kwa upande wao washindi wa kampeni hiyo wakaelezea furaha zao, pamoja na jinsi watavyotumia fedha walizokabidhiwa kufikia ndoto zao.
Kampeni hiyo iliyobebwa na kaulimbiu ya “Kila Mtu ni Mshindi”, itaendelea hadi Oktoba, ambapo kwa upande wa Washindi wa kila siku watapata Sh.100,000, washindi wa kila wiki Sh.500,000, washindi wa kila mwezi Sh. Mil 1 na washindi watano wa zawadi kuu kila mmoja atapata Sh. Mil 20.