NI MWAKA WA FURAHA KWA WASTARA

Wastara Juma,

KILA mara watu wamezoea kumuona staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma, akidondosha machozi kutokana na changamoto mbalimbali anazopitia, lakini mwaka huu 2009, ameyakataa na kusema kuwa ni mwaka wake wa furaha na mafanikio.  Wastara alisema kuwa watu wamekuwa wakimuona ni mtu wa kulia kila wakati, lakini mwaka huu ameamua kuyakataa machozi, hatalia tena anataka kuwa mtu mwenye furaha siku zote, lakini pia asiyaoneshe machungu yake kwa kila mtu kama yatazidi atalia kimoyomoyo.

“Watu wengi wameshanichukulia kuwa mimi ni mtu wa kuonewa huruma kwa yale niliyopitia, lakini nataka kuwaambia kuwa sasa nimebadilika kabisa sitaki kuyaonesha tena machungu yangu hadharani maana kuna wengine wanakukebei na siyo kukuonea huruma,” alisema Wastara.

Stori: Zaina Malogo, Dar

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO


Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment