Ni Mwendo wa Rekodi!

MAISHA yanakwenda kasi sana! Ukirudi nyuma miaka 15 katika soko la Bongo Fleva, wasanii wengi walikuwa wakitegemea kuuza kazi zao kwenye ‘cassette’, tena hapo kama siyo msambazaji Mamu Store, basi Mwananchi Store.

 

Hakukuwa na kutegemea mitandao kuwajulisha mashabiki kazi mpya, uwezo wa msanii ulikuwa ukionekana kwenye kuchezwa kazi zake redioni na kuingia kwenye chati!

 

Mambo yame badilika! Muziki unafika mbali, mitandao imekuwa ikiwasaidia sana wasanii wa Bongo Fleva na ndiyo maana si ajabu kusikia wakiweka rekodi mbalimbali ambazo hazikuwahi kuwepo na kwenda sambamba na wakali wengine duniani.

Over Ze Weekend inakuletea baadhi tu ya rekodi mbalimbali ambazo zimewekwa na wasanii Bongo na Afrika kwa jumla.

ROMMY JONES

Wiki chache zilizopita ndani ya Kiwanja cha Samaki- Samaki, Mlimani City jijini Dar, kulikuwa na bonge moja la pati ya uzinduzi wa Albam ya Changes ya DJ wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Rommy Jones ‘RJ’.

Changes ni albam yake ya kwanza na kuweka rekodi ya DJ wa kwanza Bongo kutoa albam ya Bongo Fleva.

NANDY

Kwa sasa huwezi kutaja mafanikio ya wanamuziki wa kike Bongo bila kumtaja Nandy.

Ndani ya miaka miwili mafanikio yake yamekuwa makubwa ambapo ameweka rekodi ya kuwa msanii wa kike pekee aliyefanikiwa kuanzisha tamasha la muziki (Nandy Festival) na kuwafunika mastaa wengi.

Ikumbukwe kuwa Lady Jaydee alishawahi kufanya mata masha tofauti kama la Usiku Historia ambalo lilikuwa la sehemu moja tu.

HARMONIZE

Ni mkali anayekimbiza katika Bongo Fleva akiwa ameshafanya kolabo na mastaa kibao nje ya Bongo kama Eddy Kenzo wa Uganda, Sarkodie wa Ghana, Korede Bello, Burna Boy na Yemi Alade wa Nigeria.

Harmonize anashikilia rekodi ya kuwa msanii wa kwanza Bongo kukimbiza katika Mtandao wa Youtube ambapo kupitia wimbo wake wa Kwangwaru umetazamwa na watu zaidi ya milioni 49, idadi kubwa kuliko wimbo wowote Afrika Mashariki.

DAVIDO

Ni mkali kutoka Nigeria, lakini amekubalika vilivyo. Davido ambaye alishawahi kutua Bongo katika Tamasha la Fiesta, Oktoba 2014, anashikilia rekodi ya kuwa staa pekee kutoka Afrika kufanya kolabo na staa wa kimataifa, Chris Brown.

Ikumbukwe kuwa, Davido ana kolabo nyingine za wakali wa kimataifa kama Meek Mill, Young Thug, Clean Bandit na Quavo wa Migos.

ANDREW CARLOS

 

 


Loading...

Toa comment