The House of Favourite Newspapers

Ni rahisi kugundua kama katoka kukusaliti?-2

0

Niwiki nyingine tunakutana kupitia safu hii nikiamini kwamba umzima na unaendelea vyema na shughuli zako za kila siku kama kawaida.

Mimi niko poa, tayari kukuletea muendelezo wa mada ambayo niliianza wiki iliyopita. Ninachokifanya kwenye mada hii ni kujaribu kuonesha ugumu wa kuweza kugundua pale ambapo mpenzi wako ametoka kukusaliti.
Inaelezwa kuwa, kwa ulimwengu wa sasa, ni rahisi sana mtu wako kutembea na mtu mwingine kwa muda mrefu bila ya wewe kujua. Wanaofanya hivyo wapo wengi sana huko mtaani na wewe msomaji wangu ni shahidi wa hilo.

Kipi cha kufanya?

Hakuna mbinu za wazi za kuweza kuzitumia kubaini kama mwenza wako ametoka kukusaliti, sanasana unaweza kutumia akili zako. Kama siku kajisahau karudi na ‘love bites’, hapo ndipo unaweza kujua. Au amerudi akiwa amechoka kuliko siku zote na ukimuangalia anakwepesha macho, yaani anakuwa hajiamini, jua umeibiwa.
Hapo kidogo unaweza kumtilia shaka, lakini pia anaweza kukuambia amechoka kutokana na kazi za kutwa nzima. Ndiyo maana kunakuwa na ugumu wa kugundua.

Na kwa taarifa yako sasa, hata kama atarudi na ‘love bite’ shingoni, unaweza kushangaa anakataa kabisa kwamba ametoka kufanya mambo yake, atakuwa tayari hata kuapia. Sasa mkifikia hatua hiyo utakuwa na kipi cha kushika?
Ndiyo maana tunasema, uhakika wa asilimia zote kwamba mwenza wako anakusaliti ni mpaka utakapomfuma laivu, lakini hizi dalilidalili wakati mwingine zinatupotosha.

Cha msingi hapa ni kuepuka kuishi huku ukimfikiria vibaya mweza wako. Hii kumchunguza kila wakati, kumnusa kila akirudi nyumbani, kumkagua mwili na kukimbilia simu yake akirudi nyumbani ni kujipa presha bure. Kama anakusaliti, ipo siku Mungu atakuangazia utagundua.

Lakini sasa, tukeshe tukiomba sana ili hata kama wale ambao tumetokea kuwapenda wanatusaliti, tusijue! Hivi unajisikiaje kujua kwamba mtu ambaye unampenda sana anakusaliti?
Je, ukigundua utakuwa na ujasiri wa kuchukua uamuzi wa kumuacha? Hakika ni ngumu sana kwani kumuacha mtu ambaye moyo wako umemzimikia si kazi rahisi. Ndiyo maana leo hii unaona mtu anamfumania kabisa mkewe au mumewe lakini anapiga moyo konde, anamsamehe na kuyaacha maisha yaendelee.

Hii yote ni kwa sababu, endapo kila utakapobaini kuwa unasalitiwa unaacha, basi utaacha wengi na kamwe hutapata mtu wa kutulia naye. Nasema hivyo kwa sababu hakuna utakayempata ambaye ametulia kwa asilimia zote, na kama yupo basi ni mmoja kati ya watu kumi.

Labda kwa kumalizia niseme tu kwamba kwenye mapenzi kuna sarakasi nyingi. Kusalitiwa kumekuwa kukishamiri kila kukicha kiasi kwamba huwezi kusimama leo na kujiaminisha kwamba uliyenaye hakusaliti.
Kikubwa ni wewe kujenga imani naye, kutopenda kumfuatilia sana huku kila kukicha mkikumbushana juu ya umuhimu wa kutulizana.

Madhara ya kuchepuka ni mengi kiasi kwamba ukigundua kuwa mwenza wako hatosheki na penzi lako, ana tamaa za kijinga, haoni hatari kukutengeneza ‘mtungo’, bora umuache ili asije akakuingiza kwenye matatizo makubwa.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Leave A Reply