The House of Favourite Newspapers

Ni vita ya ‘Top Four’, Siyo Mourinho na Wenger

0
Kocha wa Man United, Jose Mourinho.

KOCHA wa Arsenal, Arsène Wenger amesema anaamini mchezo wa kesho Jumapili wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United utakuwa ni vita ya kuwania kuwemo ‘Top Four’ na siyo ugomvi wa makocha.

Man United iliyo katika nafasi ya tano kwenye ligi hiyo na pointi 65, itakuwa ugenini kucheza na Arsenal kwenye Uwanja wa Emirates wakati wenyeji wapo nafasi ya sita na pointi 60.

 Kocha wa Man United, Jose Mourinho walipozinguana na Arsenal Wenger

Wenger alisema tofauti na fikra za wengi ni kwamba, mechi hiyo imejaa zaidi vita ya kuwania nafasi nne za juu kwenye ligi ili waweze kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao na si vita ya makocha.

Kwa muda mrefu, Wenger amekuwa katika vita ya maneno na Kocha wa Man United, Jose Mourinho na mashabiki wanasubiri kuona nini kitatokea dhidi ya Wenger alisema: “Nataka amani, sitaki ugomvi na mtu yeyote katika mchezo huu, wote tunawania nafasi ya kucheza Uefa, si kitu kingine na akili za watu ziwe huko siyo kwenye mambo ya ugomvi.

“Kitu cha msingi unachotakiwa kufanya wakati wa kupambana ni kuhakikisha unamshinda mshindani wako na si kitu kingine, ndiyo maana tunawaza mchezo zaidi ya mambo ya nje ya uwanja.” Vinara wa ligi hiyo, Chelsea watakuwa nyumbani keshokutwa Jumatatu kucheza na Middlesbrough, wakati jana usiku Tottenham Hotspur walicheza na West Ham United ugenini kwenye Uwanja wa London.

Leave A Reply