The House of Favourite Newspapers

NIC BENKI WAPANDA MITI 500 SHULE YA MSINGI MAJANI YA CHAI DAR

Zoezi la upandaji miti likiendelea kwenye Shule ya Msingi Majani ya Chai iliyopo Kipawa jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NIC na viongozi wengine wakipanda mti.
Meneja wa idara ya wateja wadogo na taasisi wa Benki ya NICNatasha Cathles (kushoto) akipanda mti wa matunda aina ya mwembe.
Wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Majani ya Chai.
Meneja wa idara ya wateja wadogo na taasisi wa Benki ya NIC, Natasha Cathles akizungumza jambo.

 

BENKI ya NIC, leo Mei 19 kupitia wafanyakazi wake wa benki hiyo wamepanda miti ya matunda na isiyokuwa ya matunda katika Shule ya Msingi Majani ya Chai iliyopo Kipawa jijini Dar es Salaam ili kuweza kutengeneza mazingira ya shule hiyo kuwa bora.

 

Meneja wa idara ya wateja wadogo na taasisi wa Benki ya NIC, Natasha Cathles, akizungumza katika hafla ya upandaji miti huo amesema kuwa kitendo cha benki yao kupanda miti 500 katika shule hiyo ni kuhitaji kutengeneza mazingira bora kwa ajili ya wanafunzi ili waweze kuwa katika mazingira bora na mazingira ni afya.

 

Alimpongeza mkuu wa shule hiyo kwa kukubali kitendo hicho cha kupanda miti eneo hilo na akisema kwamba hasa wamelenga kuelekea siku ya mazingira wao wakaona ni vyema kutengeneza mazingira ya wanafunzi.

Comments are closed.