NIC Waja na Tahadhari Ya Linda Mjengo Wako
Shirika la Bima la Taifa nchini (NIC) katika msimu huu wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba wamekuja na huduma mpya ya Linda Mjengo ambayo itakuwa ikilinda mjengo wako kwa gharama ya shilingi 85,000/ tu kwa mwaka.
Akizungumza na wanahabari kwenye maonesho hayo afisa wa shirika hilo, Erica Gabriel alisema bima hiyo itamsaidia mteja kuilinda nyumba yake yenye thamani ya ukubwa wowote kwa gharama ndogo ya shilingi 85,000/ tu kwa mwaka.
Amesema mteja anapokata bima hiyo itamfanya aweze kuulinda mjengo wake kwa gharama hiyo na kumuokoa endapo yatatokea madhara ya moto ambayo yameshawatia umasikini baadhi ya watu waliowahi kuungulia nyumba zao ambazo hazina bima.
Erica alisema kiwango hicho cha pesa kwa mwaka mtu yeyote anaweza kukimudu na kumfanya aishi maisha ya amani na kufidiwa mjengo wake endapo janga la moto litatokea na kuepuka umasikini wa kupoteza makazi.
Amesema kwa yeyote anayetaka huduma hiyo afike kwenye jengo lao lililopo kwenye viwanja hivyo na watamuunganisha haraka kwenye huduma hiyo pasipo usumbufu. Alimaliza kusema Erica.