The House of Favourite Newspapers

Nick Dizo ‘Mtendaji’ Nyuma Ya Video Za Hip Hop

0

nick-dizzo-1Nick Dizo.

Makala: Boniphace Ngumije

KATIKA nchi ambayo tasnia ya burudani imeshika kasi kuwa na utitiri wa watayarishaji wa muziki na video siyo jambo la kushangaza. Hivyo ndivyo ilivyo hata hapa Bongo. Hata hivyo, wingi wao, haufanyi wakali washindwe kuchomoza miongoni mwao, kama Nick Rusule ‘Nick Dizo’ anavyothibitisha.

Huyu ndiye mtendaji halisi aliyesimama nyuma ya kamera wakati kichupa cha Ibrahim Musa ‘Roma Mkatoliki’ cha wimbo wake mpya wa Kaa Tayari ukishutiwa. Pia alifanya hivyo katika wimbo wa Dangerous Boy wa Kundi la The Amazing, achilia mbali kuwa ameshafanya video mbalimbali za wasanii wakubwa Bongo, zikiwemo Nishike Mkono wa D Knob na Nakukumbuka wa Kheli Music.

Katika ‘exclusive interview’ na Risasi Vibes, Nick Dizo anafunguka mambo mbalimbali akielezea safari yake katika fani, iliyoanza mwaka 2004 kwenye mitaa ya Jiji la Dar na video yake ya kwanza kushuti ilikuwa ni ya wimbo wa DJ Kata uitwao Mama Mia. Huyu hapa!

RISASI VIBES: Wimbo huo ulikuwa na ‘impact’ gani kwako?

NICK DIZO: Ulinipa jina kwa kiasi fulani, maana nilianza kupata mashavu ya hapa na pale ya kurekodi nyimbo za wasanii wengine.

RISASI VIBES: Uliwahi kufanya kazi na Titto Baucha, mmoja kati ya madairekta wenye jina Bongo, mlikutana vipi na nini kilitokea baadaye mkaacha kufanya kazi pamoja?

NICK DIZO: Nilikutana naye mwaka 2007 katika ‘hustle’ za kutoka kwenye gemu. Baada ya kukutana tukachanganya vitu tulivyokuwa navyo kila mmoja kwa uwezo wake, kisha tukaanzisha studio iliyojulikana kwa jina la Ban Records. Yaani Ba- ilimaanisha Baucha na Nilisimama kama Nick.

Lakini baadaye kwa vile kila mmoja alikuwa na malengo yake, tukaamua kuachana kiroho safi, Baucha akafungua studio yake na kuendelea na mambo yake ya muziki, mimi nikaungana na jamaa mmoja aitwaye Sama, tukaanzisha Kampuni ya EMedia.

RISASI VIBES: EMedia ilikuwa ni ‘brand’ kubwa, unaweza kukumbusha baadhi ya nyimbo mlizofanya na nini kilitokea kampuni hiyo pia ikapotea?

NICK DIZO: Chini ya E-Media kiukweli tulipiga kazi nyingi tu na mastaa. Miongoni mwa kazi zetu ulikuwa wimbo uitwao My Baby wa Quick Rocka aliowashirikisha marehemu Albert Mangwea ‘Ngwea’

Leave A Reply