The House of Favourite Newspapers

Nicki, Meek wadaiwa kuandaa ndoa kwa siri

0

nicki-minaj-meek-mill
NEW YORK, Marekani

MASTAA Nicki Minaj na laazizi wake Meek huenda wakafunga ndoa wiki hii baada ya mtu wa karibu na Meek kufunguka kuwa mishe za shughuli hiyo zimeanza kwa siri.

Akisambaza umbea kwenye mtandao mmoja wa habari za mastaa, sosi huyo alisema ndoa ya mastaa hao inatarajiwa kufungwa jijini New York baada ya kumaliza shoo ya Tidal ambayo walitarajiwa kuifanya.

Imeelezwa kuwa, wazazi wa pande zote mbili wameridhia kufanyika kwa zoezi hilo ingawa bado haijajulikana sherehe itakuwa ya aina gani na lini kwani mambo yamekuwa yakienda kwa siri sana.

Leave A Reply