NICKI MINAJ ASEMA ‘BADO SIJAOLEWA’

MWANAMUZIKI machachari Mmarekani, Nicki Minaj, amesema bado hajapata mume wa kumuoa.  Msanii huyo ameyasema hayo majuzi kuhusiana na mpenzi wake,  Kenneth Petty, aliyemtaja kama “mume” wake katika kipindi cha mahojiano cha  “Queen Radio.” 

Habari zinasema ni kweli mrembo huyo kaangukia katika penzi na Kenneth lakini uvumi kwamba wameoana, Nicki amezikanusha licha ya kwamba kuna mipango mahsusi ya wawili hao kufunga ndoa.

Kuhusu Kenneth kuwa na historia mbaya kutokana na vitendo vingi vya kuvunja sheria, ikiwa ni pamoja na ubakaji na mauaji, Nicki amesema hilo si tatizo kwake.

Loading...

Toa comment