NICKI MINAJ ,CARDI B WADAIWA KUMALIZA BIFU
HUENDA lile bifu la muda mrefu kati ya marapa wawili wasioshikika kwenye gemu la Hip Hop kutoka Marekani, Nicki Minaj na Cardi B likawa limeisha baada ya wawili hao kutarajiwa kufanya shoo ya pamoja. Kwa mujibu wa mtandao wa Livenation ambao huandaa pia matamasha makubwa, mabosi wa wawili hao wamewekewa kandarasi mezani ya kufanya ziara ya pamoja.
“Itakuwa na manufaa kwa pande zote kwa Cardi B na Nicki,” ilisema sehemu ya mtandao huo. Endapo wawili hao watafanya shoo ya pamoja, bifu lao linalofukuta mara kwa mara mitandaoni huenda likawa ni la kutengenezwa.
Hivi karibuni, mashabiki wa Nicki walivujisha video ya wimbo mpya wa Cardi B uitwao Money jambo ambalo Cardi B aligeuka mbogo kwa kusema; “Wanasema wananichukia kumbe ndio wananipenda, wako kwenye IG (Instagram) yangu kabla hata ya mashabiki wangu, kila ninachofanya wanakijua kabla ya mashabiki wangu, hayo ndio mapenzi.”
Juzikati tena, Nicki aliingia mitandaoni na kuomba wasahau yote na wafanye kazi kwa faida jambo ambalo Cardi B naye aliingia mtandaoni na kukubaliana naye.
Comments are closed.