The House of Favourite Newspapers

Nicole: Heri Moyo Wangu Usukume tu Damu, si Vingine

0

BRIGHTON MASALU | IJUMAA | SHOW BIZ

MREMBO anayekuja kwa kasi ya 4G katika tasnia ya filamu za Kibongo, Nicole Franklin ‘The Unique’ amekiri kutokuwa na bahati ya kufurahia mapenzi, licha ya kujaaliwa urembo wa haja na kwamba hadi sasa ameamua kuuamuru moyo wake usukume damu si vingine.

Katika mazungumzo mubashara na Showbiz, msanii huyo aliyeitendea haki filamu ya Gate Keeper, akiwa sambamba na wakali kama Kajala, Ray na Rich, alisema tangu aanze kujihusisha na mapenzi, hajawahi kukutana na mwanaume mwenye mapenzi ya kweli.

“Sijui niseme nini, kila ninayemuamini huishia kuniliza, ukinitazama unaweza usiamini kabisa kama nasumbuliwa na mapenzi, wanaume wana ufundi sana wa kueleza maneno matamu kwa nje, lakini yenye kuumiza vibaya mno kwa ndani, kinachoniponza ni kumuamini mtu kwa haraka, kumpa mapenzi yote na kuvumilia hadi vitendo ambavyo havivumiliki, kwa sasa sitaki tena mapenzi, namlea mwanangu huku nikipambana na maisha,” alisema Nicole

Leave A Reply