The House of Favourite Newspapers

NIKKI WA PILI AELEZA ALIVYOKUTANA NA MCHUMBA’KE

Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’na mchumba’ke

MKALI wa Hip Hop Bongo kutoka Kundi la Weusi, Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ ameeleza alivyokutana na mchumba’ke anayetarajia kumuoa baada ya kumvalisha pete ya uchumba, Jumapili ya Desemba 9, mwaka huu.  

 

Nikki aliliambia Risasi Jumamosi kuwa alikutana na mchumba’ke huyo kwenye kongamano la ujasiriamali lililofanyika katika Ukumbi wa Millenium Tower, Kijitonyama jijini Dar.

 

“Wakati tunatoka kwenye kongamano ndipo nikamuona mtoto, nikamuomba namba huku nikijisemea mwenyewe huyu mtoto simuachi ni wa kumweka ndani kwa sababu alikuwa na vigezo vya mwanamke wa ndoto zangu,” alisema Nikki wa Pili.

Comments are closed.