The House of Favourite Newspapers

Nikki wa Pili Afungukia Maisha Yake ya Kimapenzi

STORI: ALLY KATALAMBULA | RISASI JUMAMOSI| RISASI VIBES

RAPA anayetamba na ngoma ya Sweet Mangi, Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ amefungukia maisha yake ya kimapenzi na kusema hawezi kumweka wazi mpenzi wake kwa kuwa maisha hayo ni kama maigizo.

Akipiga stori na Risasi Vibes, Nikki amesema maisha ya kuweka mambo binafsi hadharani yanamfanya aone yupo katika maisha bandia kwa kuwa eneo kubwa huwa ni maigizo.

“Siwezi kuweka wazi maisha yangu na mpenzi wangu hadharani, mimi napenda kuishi kiuhalisia, napenda kupenda na kupendwa pia, maigizo siyo kariba yangu, kuna watu wanatengeneza pesa ndefu kwa kugeuza uhusiano wao kuwa biashara, hao ni wao ila mimi siwezi,” alisema Nikki wa Pili.

 

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe nisiasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.