The House of Favourite Newspapers

Nikki Wa Pili Alizwa na Uchumi

1
Rapa wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Nikson Saimon ‘Nikki wa Pili.

Stori: Ally Katalambula | Uwazi | Habari

RAPA anayefanya poa kwenye Muziki wa Hip Hop Bongo, ambaye pia ni ‘memba’ wa Kundi la  Weusi, Nikson Saimon ‘Nikki wa Pili’ amefunguka kuwa ikiwa hali ya uchumi itazidi kuendelea kuwa ngumu na mfumuko wa bei za vyakula kupanda basi kunauwezekano mkubwa pia wa soko la muziki kudorora.

Akipiga stori na Uwazi Showbiz, Nikki aliongeza kuwa biashara yao ya muziki inategemea pia mzunguko mzuri wa uchumi maana kwa hali inavyoelekea sasa ni vigumu mtu kuacha kuangalia vipaumbele muhimu na kununua nyimbo zao mitandaoni au kuhudhuria kwenye shoo zao.

“Kwenye ukweli ni lazima tuseme ukweli. Kwa hali ya uchumi inavyoelekea sidhani kama mtu atakuwa tayari aache kununua unga wa familia yake kisha anunue nyimbo mitandaoni ama kuja kwenye shoo zetu. Kwa hiyo tunaomba tu hali ya kiuchumi iimarike ili na sisi biashara yetu iwe nzuri,” alisema Nikki wa Pili.

1 Comment
  1. […] wa muziki wa Hip Hop Bongo, Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ amempigia saluti msanii mwenzake, Ibrahimu Musa ‘R.O.M.A Mkatoliki’ kwa kusema anamkubali kwa […]

Leave A Reply