The House of Favourite Newspapers

Nikki wa pili awapa somo vijana

0

Nyota wa Hip Hop Bongo kutoka Kundi la Weusi, Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’.

NYOTA wa Hip Hop Bongo kutoka Kundi la Weusi, Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ ameibuka na kuwapa somo vijana kwamba wanatakiwa kutumia changamoto wanazopitia katika maisha na kuwa mafanikio kuliko kukaa na kulaumu.

kipiga stori na Risasi Vibes, Nikki wa Pili anayebamba na Ngoma ya Baba Swalehe alisema, vijana wengi wamekuwa na dhana kwamba wakishasoma wanategemea kuajiriwa tu kitu ambacho siyo kizuri na kinaweza kuwagharimu kwani ajira kwa hapa nchini zipo chache hivyo ni vyema wakatumia changamoto za ajira kuwa mafanikio kwao.

“Vijana tunatakiwa tuamke hata kama umesoma mpaka wapi usitegemee kuajiriwa tu kwa sababu utaishia kukaa kijiweni ukisubiri ajira na mwishowe unakuwa muhuni wa mtaani, ni vyema tukajiajiri wenyewe hiyo itatusaidia kuendesha maisha yetu ya kila siku,” alisema Nikki wa Pili.

Leave A Reply