The House of Favourite Newspapers

Nikki wa Pili: Sijawahi kuwaza kutoka Weusi

0

UKIZUNGUMZIA wanamuziki wasomi Bongo, huwezi kumuepuka Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’, ni moja kati ya wasanii wa Hip Hop kutoka kwenye Kundi la Weusi.

 

Mbali na muziki, kwa sasa Nikki anavaa pia kofia ya mhamasishaji kwani amejizolea umaarufu mkubwa kwenye majukwaa ya Fursa yaliyokuwa yanaratibiwa na Clouds Media Group.

Mikito Nusunusu imezungumza naye, amefunguka mengi hapa:

Mikito: Nikki tunafahamu sasa hivi kuna janga la Corona, vipi kwa upande wako limekuathiri kiasi gani?

 

Nikki: Janga hili limetuathiri sana wanamuziki kwa sababu sisi tunategemea sana shoo na mikusanyiko imekatazwa, hivyo cha muhimu ni kusimama na kumuomba Mungu atuepushe na janga hili.

Mikito: Kwa sasa hivi kuna biashara yoyote unaifanya ili kuweza kujipatia kipato?

Nikki: Kwa sasa mimi natumia jina langu kama Nikki kwa kujipatia kipato, ukiachana na kufanya shoo, mimi nafanya kazi ya Digital Platform, nimekuwa Ambassador wa DSTV.

 

Kwa hiyo nafanya biashara nao, pia ninayo Smart Generation, hivyo wasanii wangepaswa kutumia majina yao kujipatia kipato.

Mikito: Una mikakati gani ya kufanya ili usipoteze mashabiki wako, pia usipoteze jina lako?

Nikki: Ni kuendelea kufanya kazi kwa bidii sana pia uwe unafanya Insta live ili uwe unaongea na mashabiki wako.

Mikito: Muziki wa sasa umekuwa na ushindani mkubwa sana, ni njia gani unatumia kuhakikisha haushuki kimuziki?

Nikki: Kweli ushindani nafikiri upo kila siku wala siyo mwaka huu na kuendelea kukaa kwenye muziki ni kufanya muziki mzuri na pia kuendelea kutengeneza brand yako zaidi kama mimi brand yangu naifanyia kwenye miradi miezi miwili iliyopita nilikuwa kwenye Kipepeo karibu nchi nzima na sasa hivi ninaproject ya Sitetereki kama Director na pia tuna mikakati ya kuanzisha project inayoitwa Naweza.

 

Mikito: Kwa sasa tumeona wasanii wengi wamekuwa na mtindo wa kutoa albamu fupi (EP) kwako hiyo imekaaje?

 

Nikki: Kuhusiana na EP kuna album ya Weusi sisi kama kundi inakuja, kwa hiyo baada ya hiyo inaweza ikaja album yangu mwenyewe.

 

Mikito: Je, ushawahi kuwaza kuachana na kundi la Weusi na kujisimamia mwenyewe kama Nikki?

 

Nikki: Kuhusiana na mimi kutoka Weusi sijui kwa sababu Weusi ni zaidi ya kundi na sisi ni kama ndugu, kwa

 

hiyo huwezi kuachana na ndugu zako.

 

Hivyo mimi Weusi nitakuwepo sana tu.Mikito: Muziki wa makundi umekuwa na migogoro mingi, kwa upande wako unalizungumziaje suala hili?

 

Nikki: Migogoro kwenye makundi yapo ila cha msingi ni kukubaliana katika terms ambazo ni za kisheria kila mtu ajue nafasi yake, share yake.Mikito: Vipi kuhusiana na kolabo za Kimataifa?

 

Nikki: Tumeshafanya kolabo nyingi na nyingine zinakuja, tuna kolabo na Simi kutoka Nigeria, pia Sauti Solo. Kwa hiyo, Corona ikipita mambo yatakuwa sawa.

 

Mikito: Changamoto gani kubwa unazipitia kwenye muziki wako kwa sasa?

 

Nikki: Ni zile zile ambazo wasanii wengine wanazipitia kama challenge ya kubadilisha muziki kuwa biashara pia na kutumia jina kuweza kujiajiri.

Mikito: Na mafanikio gani ambayo unajivunia kupitia muziki?

 

Nikki: Mimi naishi kwa kupitia muziki na nimesoma kwa kupitia muziki, nina mali zangu kupitia muziki na vitu vyangu vyote ninavyovifanya ni kwa sababu ya muziki, kwa hiyo hayo ndiyo mafanikio yangu kupitia muziki.

 

Mikito: Neno la mwisho kwa mashabiki zako.

 

Nikki: Nawapenda sana, wazidi kunisapoti maana bila wao mimi siyo kitu

Leave A Reply