Nilifanya Mapenzi na Maiti 20 Ili Nitajirike 028
ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA
Wote tukabaki kimya na baada ya muda kama wa dakika mbili, watu wawili wakatokea, walikuwa ni mwanamke na mwanaume. Wote walikuwa wazuri wa sura, sikujua hao walikuwa akina nani lakini tukaambiwa kwa sisi tusiowajua, hao walikuwa ni jini mahaba ambaye alijulikana kwa jina la Maimuna na jini Makata, jini aliyekuwa na hasira kali sana.
ENDELEA NAYO…
Hao ndiyo waliokuwa wakiuendesha ulimwengu kwa kipindi hicho, wao ndiyo walifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha dunia inapotea. Leo unapowaona watu wanapenda sana ngono, jua kwamba Jini Maimuna anafanya kazi yake, anawasahaulisha watu na ufalme wa Mungu hivyo kuanguka katika dhambi.
Mbali na ngono, pia unaweza kushangaa kwa nini watu wanauana sana. Unasikia mahali fulani kuna mauaji makubwa yametokea, kesho unasikia kuna mauaji sehemu fulani, ndugu zangu, hizo ni kazi za huyu Jini Makata ambaye amekuwa akisimamia katika suala zima la mauaji.
Walikuwa hapo kwa ajili ya kuwapongeza, walifanya kazi kubwa sana kiasi kwamba hata shetani mwenyewe alihisi jina lake linaendelea kutukuzwa kila siku.
Walianza kuongea, hawakuongea Kiswahili wala Kiingereza, walizungumza kwa lugha nyingine kabisa ambayo sidhani kama ilikuwa hapa duniani lakini kitu cha ajabu, niliielewa vizuri lugha hiyo.
Walipata dakika ishirini za kuzungumza ndipo wakaondoka na baadaye shetani kuingia. Kama unakumbuka ile picha niliyoiona pale nje kwenye jengo, ndiyo picha halisi ya shetani, alikuwa na umbo la kibinadamu lakini sura yake ilikuwa ni ya mnyama.
Alisimama mbele yetu na kuanza kuzungumza, sauti yake haikuwa ya kawaida, ilikuwa na mikwaruzo mingi, sauti yake ilikuwa tofauti na ile sauti ya kipole iliyokuwa imezungumza nami siku za nyuma, kwa kuisikia sauti yake tu, ilikuwa ni rahisi kujua kwamba huyo hakuwa mtu wa amani hata kidogo.
Huko ndipo nilipopata siri kubwa, ningependa nizungumze japokuwa wengine wanaweza kuhisi vibaya. Katika dini hiyo kumegawanyika, kuna watu ambao kazi yao kubwa inakuwa ni kusimamia wanamuziki wa kike ambao wanatakiwa kuitumia miili yao kuvutia kazi zao.
Angalia video za muziki nchini Marekani, wanamuziki wengi wa kike wanacheza huku wakiwa wamevalia mavazi nusu utupu, hawafanyi hivyo kwa kupenda bali wamepewa maagizo kutoka katika dini hiyo ambayo imekusanya watu wengi sana duniani.
Siku hiyo ilikuwa ni siku ya kupewa maagizo ya kufanya na vilevile kufahamiana na watu wengine huku wageni tukikaribishwa. Tulikaa huko kanisani kwa saa mbili ndipo tukatawanyika na kurudi.
“Mungu! Nitawezaje kutoka humu?” nilibaki nikiuliza kana kwamba Mungu alikuwa mbele yangu.
“Sipendi kukaa humu ila napo dunia imenikamata Mungu, nitatokaje?” niliendelea kuuliza huku nikiamini Mungu angenisikia na kunipa jibu.
Njiani wakati naelekea hotelini nilikuwa na mawazo tele, kiukweli hakukuwa na kitu kilichokuwa kikiniumiza kama kuwa katika dini hii, nilishindwa kujitoa kwa sababu nilitamani ule utajiri waliokuwa wamenipa.
Sikuchukua muda mrefu njiani nikafika hotelini, nikateremka na kupanda lifti kisha kuelekea chumbani kwangu huku ikiwa ni saa tisa usiku. Niliposhuka kwenye lifti, nikateremka na kuanza kuufuata mlango, nilipoufungua, nikaingia ndani na kuwasha taa.
Nilishtuka sana baada ya taa kuwaka, nilimuona Majeed akiwa mbele yangu, alikuwa kwenye kiti, alionekana kuwa mwingi wa hasira, alikuwa akiniangalia huku akiuma meno yake kwa hasira.
Niliogopa sana, nikabaki nikitetemeka, kwanza nikajiuliza aliingiaje ndani, hakuwa na ufunguo, funguo zote nilikuwa nazo mimi na pia nyingine iliyokuwa mapokezini, haikuchukuliwa kwani kama ingechukuliwa ningejua tu.
Wakati nikijiuliza aliingia vipi ndani ya chumba hicho, Majeed akasimama na kuanza kunisogelea, alionekana kuwa katika hali isiyo ya kawaida, niliona sura yake ikibadilika rangi na kuwa nyekundu, niliogopa, sikujua alitaka kufanya nini, lakini kingine nilichojiuliza ni binadamu gani alikuwa na uwezo wa kubadilika rangi na kuwa mwekundu? Sikupata jibu, kila alivyokuwa akinisogelea, nilitamani kukimbia.
***
Kwa kweli niliogopa sana, sikuwahi kumuona Majeed akiwa kwenye hali ile tangu nilipofahamiana naye, alionekana kukasirika sana na sikujua sababu ya yeye kuwa vile ilikuwa ni nini. Nilibaki nikitetemeka huku nikimsogelea.
Nilipomfikia, nikamshika, mwili wake ulikuwa na joto kali sana, si kama watu waliokuwa wakiumwa miili yao ilivyokuwa bali ulikuwa na joto kali kiasi kwamba mpaka nikahisi naungua hivyo kuutoa mkono wangu haraka sana katika mwili wake.
“Kuna nini?” nilimuuliza huku nikionekana kuogopa.
“Umetoka wapi?” aliniuliza huku akiniangalia usoni.
“Kutembea…”
“Niambie umetoka wapi,” aliniambia huku akisimama.
“Kwa nini unaniuliza hivyo?” nami nilimuuliza.
“Ninataka kujua, umetoka wapi?” aliniuliza tena.
Kwa kweli alinikera sana, ndiyo nilikuwa nampenda lakini hakutakiwa kuwa mkali kama alivyokuwa. Mimi ni mwanamke, ninahitaji mwanaume atakayekuwa tayari kukaa chini na mimi na kuzungumza, pale ninapokosea, basi aniambie kwa sauti ambayo itanifanya nijue kweli nimekosea.
Yeye alikuwa mpenzi wangu, lakini hakupafahamu nyumbani kwangu, tulikutana tu ndani ya ndege, baada ya hapo, hakukuwa na kingine kilichoendelea, sasa kwa nini alijifanya kuwa mkali kwangu?
“Unaniuliza hivyo kama nani?” nilimuuliza kwa ukali.
Nilimuuliza hivyo kwani kama ningekaa kimya, angenipanda kichwani.
Kutokana na swali hilo, nikamuona akianza kunyong’onyea na kukaa chini. Alikubaliana na swali langu, hakuwa mtu wa kunipelekesha ni lazima ajue kwamba mimi kama mwanamke nilikuwa na nafasi yangu katika uhusiano na si kufanya kila alichotaka nikifanye.
Kila mtu ananafasi yake ktk mahusiano