The House of Favourite Newspapers

Niliolewa na Mganga kwa Tamaa ya Cheo Kazini-35

0

ILIPOISHIA:

Kila aliponisugua alinieleza nijimwagie maji nami nilifanya vile, alipomaliza kichwani alihamia mabegani na kunisugua na mimi kujimwagia maji. Kazi ilikuwa ngumu alipokuwa akinisugua kifuani hasa kwenye matiti, yule mzee alikuwa kama anafanya makusudi kwa kunisugua kama ananitomasa.

SASA ENDELEA…

Pamoja na kuwa kwenye tiba hali yangu ilikuwa mbaya na kutamani nimuombe mzee Sionjwi apunguze angalau kidogo hali yangu iliyokuwa mbaya sana. Asikuambie mtu sisi wanawake tuna wakati mgumu sana tunapokutana na waganga wa kiume hasa katika tiba inayohusu kuguswa sehemu zenye mihemko.

Wakati huo nilihisi mwinuko chini ulionigusa  niliamini kabisa hata babu hali yake haikuwa nzuri.  Niliamini kwa mwanaume yoyote shababi hawezi kustahimili kuugusa mwili kama wangu na kubakia vilevile. Umbile langu hata likiwa kwenye nguo lilikuwa utata mtupu itakuwa nimevua nguo zote na kujifunga kanga ambayo nayo ilikuwa imeloa na kuganda mwilini.

Ajabu nyingine babu alipokuwa akinisugua kifuani aliganda eneo moja la matiti kwa muda mrefu huku akitoa pumzi za kushikika. Wakati huo mwili wangu nao ulikuwa kwenye hali mbaya sana na kuhisi miguu kutetemeka kwa ashki. Hata sikuelewa kilichoendelea zaidi ya kujikuta katikati ya kilele cha burudani.

Mtoto nilisahau kabisa kama nipo kwenye tiba kwani nilikuwa na muda mrefu sijakutana na shuruba pevu kama ile. Tiba ilibadilika na kuwa penzi zito lililokata kiu yangu mpaka tunaachiana mwili niliusikia mwepesiii. Moyoni nilipanga kama nitakwenda kusoma basi nitahakikisha hata nikiolewa lazima niwe nakutana naye hata mara moja kwa mwezi.

Baada ya mtanange wa kukata na shoka kwenye majani na zoezi kubadilika babu alinieleza kuwa tiba imeharibika hivyo tulitakiwa kurudia zoezi lile siku ya pili muda kama ule.

“Babu huoni muda unakwenda?”

Japokuwa ilikuwa mwisho wa wiki niliona kama naweza kuchelewa kama mchezo ule utaendelea na kujikuta badala ya tiba ingegeuke kijiwe cha kufanyia mapenzi na kupoteza maana yote ya mimi kufunga safari kufuata tiba.

“Hatuna jinsi tukilazimisha tutaharibu kila kitu.”

“Sasa babu kama ulijua hivyo kwa nini umekubali kufanya mapenzi?”

“Mjukuu, huwezi kuamini hata mimi sijui ilikuwaje zaidi ya kujikuta katikati ya safari.”

“Kwani tukioga na kuanza upya kuna nini?”

“Mzimu umekasirika badala kufanya kilichotupeleka tumechafua kazi. Kwa leo haiwezekani tena baada ya kuuita ulifika kwa ajili ya kusikiliza shida yetu  lakini kitendo tulichokifanya umekasirika na kuondoka.”

“Ha! Babu huoni tumeharibu kila kitu sasa tutafanyaje kama tumeuudhi mzimu?” nilishtuka kusikia tumeuudhi mzimu ambao ulifika kutusikiliza shida yetu lakini tukaudharau kwa kufanya mapenzi mbele yake tena kwenye sehemu yake inayoiheshimu.

“Ni makosa ya kawaida katika kazi.”

“Sasa itakuwaje?”

“ Hiyo niachie mimi.”

“Lakini babu taratibu za huku unazijua vizuri, mimi na wewe nani mganga?”

“Mganga mimi, ndiyo maana nikakuambia kesho tunarudia zoezi.”

“Mzimu utakubali?”

“Nimekueleza kazi yote niachie mimi, hii si mara ya kwanza kutokea kitu kama hiki, najua namna ya kurekebisha. Kesho tutakuja na kuku mwekundu tutamchinja kabla ya kazi kila kitu kitakuwa sawa.”

Kauli ya babu ilionesha kabisa ule ulikuwa mchezo wake alipowapeleka wanawake katika zoezi la kuwaosha. Hali ile ilinitisha sana kuonesha babu atakuwa ametembea na wanawake wengi kibaya bila kondomu. Lakini sikutaka kuuliza kitu kwa vile nilimjua lazima tungetibuana nilikaa kimya na maswali yangu moyoni.

“Sasa vipi na kesho ikitokea kama leo itakuwaje?”

“Kesho nitatumia njia nyingine ambayo haitatuingiza kwenye vishawishi vya ngono.”

“Kwa nini hukuitumia leo?”

“Hii niliyotumia ni njia fupi unafanya vitu viwili kwa wakati mmoja, lakini kilichotokea ni bahati mbaya kwa vile hata mimi mwanadamu pamoja ni mganga nina roho ya matamanio kama wengine.”

“Mmh!” nilijilaumu kuacha kilichonipeleka na kuingia kwenye kitu kingine kilichofanya tuharibu zoezi lililonitoa mjini kwenda kugeuza matokeo ya mimi kwenda kusoma nje ya nchi.

Lakini kwa upande wa pili mzee alinitendea haki kwa kunikata kiu ya muda mrefu kukutana na mwanaume mwenye nguvu kama faru. Umri wa babu na kazi aliyonifanyia vilikuwa vitu viwili tofauti.

Baada ya zoezi  kuharibika  tuliahirisha tiba na kukubaliana kazi ile tuifanye kesho yake. Baada ya kuoga na kila mtu kuvaa nguo zake tulianza safari ya kurudi nyumbani. Njiani nilimuuliza babu kuhusiana na uwezo wake wa kuweza kumridhisha mwanamke tofauti na umri wake wakati kuna vijana wadogo hawana nguvu kama zake.

“Babu kuna siri gani ya umri wako na nguvu ulizonazo?”

“Mjukuu sisi watu wa zamani hatuli vitu vya kutengeneza tunakula chakula cha asilia pia hata dawa zetu zina nguvu hazichanganywi na kitu cha kuipunguza nguvu.”

“Unawezaje kuwaridhisha wanawake wote tena vijana?”

“Kwa vile nina uwezo, ukiona kapu linaendelea kuingia vitu ujue bado lina nafasi.”

“Babu hapo umeniacha njia panda unamaanisha nini?”

“Ukiona mimi mzee nachukua wasichana wadogo ujue uwezo wa kuwahudumia ninao. Naweza kugawa dozi kwa kila mmoja kila siku, lakini sasa hivi kila mmoja anapata siku mbili anamuachia mwenzake ila anayeshikika kwa dharura huwa anapata huduma ya kwanza.”

“Mmh! Kweli wewe kiboko.”

“Kwani we umeonaje?”

“Mmh! Temea chini babu umekamilika.”

“Basi mjukuu, kama babu hakufikishi kuna dawa nitakupa utamwekea kwenye chai, nakuhakikishia tabu zote zitaisha nawe utafaidi  kama wenzako.”

“Nitashukuru babu, lakini baada ya kurudi safari yangu, naogopa nikimwekea sasa hivi na mimi kuondoka nitakuwa nawatengenezea wengine huenda nikirudi asiwe wangu.”

Itaendelea wiki ijayo.

Leave A Reply