Niliondoka Kama Mkimbizi, Niliazima Ada ya Mwanafunzi – Video

Mwanamasumbwi Hassani Mwakinyo aliyeweka historia baada ya kumtwanga Muingereza, Sam Eggington, leo ametembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwaahidi Watanzania kuwa hawatawaangusha katika mashindano mengine ambayo yapo mbele yake.

 

Akizungumza na wanahabari nje ya ukumbi wa Bunge hilo jijini Dodoma, Mwakinyo amesema jambo ambalo hatolisahahu katika ushindi huo wa juzi ni pale alipiokuwa akitafuta visa kwa ajili ya kusafiri kwenda Uingereza kwenye mpambano huo.

 

“Nimeondoka Tanzania kama mfungwa, kama mkimbizi, hata pesa ya kulipia visa ilikuwa shida kuipata, nakumbuka hata nauli tu ilibidi nikope pesa ya ada ya mwanafunzi.

 

“Nimepigana Uingereza bila sapoti yoyote, lakini namshukuru Mungu nimeshinda, wapo wengi wanasema ni mameneja wangu, niseme tu kwamba ni waongo, hakuna mtu anayenimeneji, wala aliyetoa pesa yake mfukoni kunigharamaia,” amesema Mwakinyo.

 

VIDEO: MSIKIE HAPA AKIFUNGUKA

Loading...

Toa comment