PICHA: Wakenya Wanasema Huyu Ni Copy Paste Ya First Lady Mama Margaret Kenyatta

Kwenye zile za watu kufananishwa na mastaa au watu wengine wakubwa na maarufu duniani ongeza na hii ya huyu mama anayefananishwa na First Lady wa Kenya, Mama Margaret Kenyatta.

Nimekutana na stori kwenye mtandao mmoja wa Kenya ya mama mmoja aitwaye Margaret Aswani anaedaiwa kufanana sana na mke wa Rais wa Kenya, Mama Margaret Kenyatta.

Kwa mujibu wa mtandao huo, Mama Aswani amekuwa akipewa msaada na upendeleo fulani kwenye sehemu mbalimbali za umma kama vile Supermarket, Benki, na sehemu nyingine kutokana na watu kumfananisha sana na First Lady wa nchi hiyo Margaret Kenyatta.

Kushoto: Mama Margaret Aswani & Kulia: First Lady wa Kenya Mama Margaret Kenyatta.

Mwaka 2015 mama Aswani alihudhuria shererhe za Marathon za ‘Beyond Zero Marathon’ na kuwachanganya Wakenya wengi waliostajabishwa na kufanana kwa mama huyo na mke wa Rais wa nchi hiyo.

Je, wewe unaonaje, ni kweli mama Margaret Aswani kafanana na First Lady Mama Margaret Kenyatta? Niahcie comment yako hapa chini.

 

IMEANDIKWA NA: Sandra Brown.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, muziki na nyingine zikufikie kwa wakati.

 

 

 
Toa comment