The House of Favourite Newspapers

Nimelea Vipaji Vingi Bongo Movies-Lamata

0

MTAYARISHAJI maarufu wa Tamthiliya Bongo, Lamata na mmoja wa waigizaji wake kwenye Tamthiliya ya Juakali, Dorah, leo wamezungumza mambo mengi juu ya kazi yao ya uigizaji ndani ya Kipindi cha Hotpot cha +255 Global Radio na Global TV kwenye mahojiano maalum yaliyofanyika katika Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza-Afrikasana jijini Dar.

 

Lamata; miongoni mwa mambo aliyoyazungumza ni namna alivyolea na kukuza vipaji vingi vya Bongo Movies na kuwa na idadi kuwa ya filamu alizoziongoza ambazo wakati mwingine anasahau idadi yake.

 


“Nimeongoza filamu nyingi sana, kuna siku nilikuwa ninahesabu zikafika kama 65 hivi,unajua watuwengi hawakunijua tangu mwanzo kwa sababu mimi siyo mtu wa mbele ya kamera,” amesema Lamata na mengine mengine mengi.

 

Kwa upande wake, Dorah amesema kuwa, mambo mengi anayoigiza kweny tamyhiliya ni sehemu ya maisha aliyopitia ya unyanyasaji na kudharauliwa kutokana na maumbile yake.

 

Leave A Reply