The House of Favourite Newspapers

Ningekuwa mimi Dudu Baya….!

UKIINGIA katika mitandao ya kijamii kila kona, iwe ni Facebook, Instagram, Twitter au Youtube, msemo Konki Konki Konki Master si mgeni.

Msemo huo mwanzilishi wake ni mkongwe wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ na umeanza kusambaa siku chache baada ya kujirekodi kipande cha video na kutaja listi ya mashoga akianza na kusema na kumalizia Konki Konki Konki Master.

Gumzo limekuwa kubwa na msemo huo umegeuzwa na kuwa wa kiburudani zaidi na wengine wameanza kuiga kwa kuweka vipande vya video wakiwataja watu kwa mtindo wa kufurahisha ‘genge’.

Kwa kutambua msemo huo, zipo fursa ambazo kama mimi ningekuwa Dudu Baya, basi sasa hivi ningekuwa naogelea mihela kupitia fursa hizo ambazo ni;

  • Youtube

Kwa kuwa nina uwezo wa kujirekodi vipande vya video, basi ningerekodi vipande vingi vya video tena siyo vya kuwataja mashoga bali vingekuwa vya kufurahisha watu tu bila kulisahau jina langu la Konki Konki Konki Master kwenye kila video kisha

natupia katika Mtandao wa Youtube ili kupata ‘views’ za kutosha na mwisho wa siku, natengeneza mkwanja kupitia views hizo.

  • Matangazo ya kibiashara

Najua watu wengi wanapenda kutangaza biashara zao; hii ingekuwa fursa kwangu ya kuzimeki. Kwanza kila biashara ningewatangazia huku nikianza na kumaliza na jina la Konki Konki Konki Master.

Ningetengeneza tisheti zangu na kofia zenye jina la Konki Konki Master, unafikiri vijana wa leo wanaotaka kwenda na wakati wangeacha kununua na kuzivaa? Ningekuwa nimewakamata tu!

  • Muziki

Kwa kuwa kwenye muziki wa Bongo Fleva ni kama niliupa kisogo na kusemekana nimepotea, kwa sasa ninafuatiliwa kila kona kwa hiyo hii ingekuwa njia ya kunirudisha. Ni bonge la kiki, yaani kwanza ningetengeneza wimbo na kuuita Konki au Konki Master na ningetaja hata makonki wenzangu kwenye muziki mwanzo mwisho, unafikiri nani asingesikiliza? Wangesikiliza na shoo za kumwaga!

  • Ubalozi

Najua kuna ushindani mkubwa wa kibiashara katika makampuni nchini. Kuna maduka makubwa ya nguo, simu na sasa hivi hadi makampuni ya michezo ya kubahatisha ya betting.

Hata kwa kujipendekeza ningewasiliana nao na kuwa balozi mzuri kwa kuwatangazia biashara zao nikianza au kumaliza na jina la Konki Konki Konki Master. Unadhani wasingekubali? Wangekubali na ningepiga bingo za kutosha!

Kwa maoni nicheki kupitia 0713 750 910.

 

MAKALA: ANDREW CARLOS

Comments are closed.