Kartra

Ninja Awasikilizia Madaktari Yanga

BEKI wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amefichukua kwa sasa anaendelea kupata huduma ya matibabu kutokana na kusumbuliwa na tatizo la misuli, huku akisisitiza anasuburi kauli ya madaktari aweze kurejea uwanjani.

 

Ninja ametoa kauli hiyo baada ya kukosekana katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara ambapo pia ataukosa mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Mwadui unaotarajiwa kupigwa keshokutwa Jumanne kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ninja alisema kwa sasa anaendelea na matibabu, lakini hajui lini atarejea uwanjani kwa kuwa tatizo lake lipo chini ya uangalizi wa daktari wa timu hiyo.

 

“Sijui siku gani nitarejea uwanjani, lakini jambo kubwa bado naendelea kupata matibabu kutokana na tatizo linalonisumbua, lakini namshukuru Mungu hadi sasa nipo sawa licha ya kwamba bado tiba haijaisha.

 

Nadhani nitaiwahi mechi ya Simba, lakini bado kila kitu kinahitaji maombi namna matibabu yanavyokwenda maana hata ukiangalia tupo kwenye ushindani mkubwa wa kupigania ubingwa wa ligi kuu kutokana na mechi ambazo zimebaki,” alisema Ninja.

STORI: IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam


Toa comment