Ninja: Hii siyo Yanga Ninayoijua

BEKI wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, ameibuka na kukiri wazi kuwa anapata tabu kutokana na ugumu wanaopitia kwenye Ligi Kuu Bara huku akisisitiza wazi haioni Yanga aliyokuwa ameizoea kwani imekuwa ikiwavunja moyo kadiri muda unavyokwenda.

 

Ninja ambaye amekuwa hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, mara ya mwisho akionekana uwanjani katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, Januari, mwaka huu, ametoa kauli hiyo kutokana na matokeo ya sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ninja alisema kuwa kwa sasa wanapitia kipindi kigumu kutokana na kushindwa kuelewa wamepatwa jambo gani kwa kuwa wanacheza chini ya kiwango.

 

“Kiukweli hata mimi sielewi kwa nini tunacheza hivi kwa sababu katika mazoezi tunacheza vizuri na ari ya wachezaji ipo juu na hata kwenye mechi wachezaji bado tunaonekana tuna ari ya kupambana lakini mambo yanakuwa nje ya matarajio yetu.

 

“Binafsi hii siyo Yanga ambayo nimeizoea kuiona inacheza, mambo yamekuwa magumu mno upande wetu licha ya kuwa tunapambana kuhakikisha timu inafikia malengo lakini sijui jambo gani linatukumba,” alisema Ninja.


Toa comment