The House of Favourite Newspapers

NINJA, MAKAMBO WAIMALIZA BIASHARA UTD – VIDEO

Kikosi cha Yanga kimeendeleza rekodi yake ya kucheza bila kupoteza mchezo katika Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya Biashara United mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa.

 

Bishara United walifanikiwa kupata bao dakika ya 37 lililofungwa na Abdulmajid Mangalo hali iliyowafanya Yanga kusubiri kupata matokeo kipindi cha pili cha mchezo huo.

 

Kipindi cha pili Yanga walifanikiwa kusawazisha bao kupitia kwa beki wao Shaibu Ninja dakika ya 70 na kuweza kufanya usawa kwenye mchezo huo hali iliyowapa zaidi nguvu wachezaji wa Yanga.

Dakika ya 80 Herieter Makambo aliandika bao la pili la ushindi kwa kumpiga chenga Abdulmajid Mangalo na kufanikiwa kufunga bao la pili kwa kutumia mguu wa kulia.

 

Kwa ushindi huo Yanga wanarejea kileleni kibabe wakiwa na jumla ya pointi 41 na kuwaacha wapinzani wao Simba kwa jumla ya alama 14 ambao wana michezo mitatu mkononi ili kuwa sawa kimichezo na Yanga.

MAGOLI ya YANGA VS BIASHARA UTD 2 -1

Comments are closed.