The House of Favourite Newspapers

Nisamehe Latifa-44

0

ILIISHIA WIKI ILIYOPITA

Latifa ameingia ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kuzitembelea hospitali mbalimbali. Anapofika huko, anajikuta akiangukia katika penzi la Dominick na uhusiano wa kimapenzi kuanza kati yao.

ENDELEA NAYO…    

Kwa mara ya kwanza Dominick akajikuta kifuani mwa Latifa, wakabaki wamekumbatiana kitandani na baada ya dakika chache, kelele za kitanda na sauti za mahaba zikaanza kusikika chumbani humo. Penzi jipya likafunguliwa huku kila mmoja akimuahidi mwenzake kwamba hatakuja kumuumiza katika maisha yao ya kimapenzi.

****

Bi Rachel alikuwa na furaha tele, kila alipomwangalia Latifa ambaye alifika nchini Tanzania kwa ajili ya ziara yake ya kuwatembelea Watanzania wengine, moyo wake ukafarijika mno.

Kila wakati alikuwa akitazama televisheni, alimkumbuka msichana huyo, aliishi naye, yeye ndiye aliyempeleka nchini Marekani ambapo huko alisoma na binti yake, Dorcas, leo hii, yule Latifa maskini, mtoto aliyezaliwa na mwanamke mnywa gongo alikuwa maarufu duniani, tena mwenye fedha nyingi.

Baada ya Latifa kutembelea hospitali hizo, akapigiwa simu na msichana huyo na kumwambia kwamba alitakiwa kujiandaa kwani walitakiwa kuonana katika Ofisi za Kituo cha Televisheni cha Global kwa ajili ya kuzungumza mengi.

Bi Rachel alifurahi kusikia hivyo, akahisi kuthaminiwa zaidi ya mtu yeyote yule. Alichokifanya ni kuwasiliana na mzee Issa na bi Semeni ambao hao ndiyo waliomlea Latifa kule Manzese, ila katika kipindi hicho, hata wao maisha yalikuwa mazuri hasa mara baada ya Latifa kuwa bilionea.

Saa sita mchana, gari la kifahari likaanza kuingia katika eneo la kituo hicho, mlango ukafunguliwa na Latifa kuteremka, akaanza kutembea kuelekea ndani ya jengo hilo. Alipoingia ndani na kuwaona ndugu zake, kwa furaha akawakimbilia na kuwakumbatia, machozi ya furaha yakaanza kumtoka.

“Nashukuru sana mama, nashukuru sana mama kwa msaada wako, bila wewe, nisingekuwa hapa,” alisema Latifa huku akiwa amemkumbatia bi Rachel.

“Usijali Latifa, nilifanya yote kwa kuwa nilihisi kukusaidia,” alisema bi Rachel.

Wafanyakazi wote waliokuwa mahali hapo wakaanza kuwaangalia watu hao, kumuona Latifa katika ofisi zao walijisikia fahari sana, wengine wakachukua nafasi hiyo kupiga naye picha na kuzirusha mitandaoni.

Baada ya kumaliza ishu ya kupiga picha na wafanyakazi, akaitwa katika chumba kimoja ambacho kilikuwa maalum kwa ajili ya kufanya mahojiano ambayo yangerushwa moja kwa moja kwenye televisheni.

“Karibu Latifa,” alikaribishwa.

Akaanza kufanyiwa maandalizi kwa ajili ya uchukuaji video, muda huo, ndugu zake walikuwa pembeni wakifuatilia kila kitu, walionekana kuwa na furaha mno. Dominick hakuacha kuchukua kila kitu kilichokuwa kikiendelea mahali hapo, bado aliendelea na mchakato wake wa kumtengenezea makala msichana huyo. Baada ya kumaliza, akaitwa mbele ya kamera na kuanza kuhojiwa.

Latifa akaanza kusimulia historia ya maisha yake tangu mama yake alipofukuzwa historia yake alisimuliwa na mzee Issa.

Je, kilifuatia nini? Usikose mwendelezo wa simulizi hii tamu wikim ijayo.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

globalbreakingnews.JPG

Leave A Reply