The House of Favourite Newspapers

NISHA Afunguka Kibenteni Kilivyomtesa

Salma Jabu ‘Nisha’

STAA wa filamu na muziki Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amefunguka jinsi alivyoteswa na penzi la mwanaume mwenye umri mdogo ‘kibenteni’ kutokana na kumgeuza ‘ATM’ kwa kumuhudumia kama mwanaye.

Nisha aliiambia Za Motomoto News kuwa wakati akiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na kibenteni huyo ambaye hakutaka kumtaja jina alikuwa akimnunulia kila kitu na kumpa fedha na kumuhudumia kama mtoto wake lakini baadaye alikuja kushtuka kuwa anachunwa na kua­mua kuachana naye.

“Nimejifunza sana na nime­koma kuwa na uhusiano na mwanaume ninayemzidi umri na kipato maana nilijikuta nime­ingia kwenye uhusiano huo bila kujua kwamba kibenteni huyo ni tege­mezi ambaye alinifanya kama mashine yake ya ATM na kuniko­moa kuja kushtuka ameshanikwan­gua vya kutosha,” alisema Nisha.

Hata hivyo Nisha aliwataka mastaa wa kike kuwa makini wanapoing­ia kwenye uhusiano kwani kwa sasa kuna wanaume vibenteni ambao wanatafuta wanawake wanaowazidi kipato na umri wakiwa na dhu­muni la kuwachuna fedha zao.

Stori : NA GLADNESS MALLYA

Comments are closed.