USICHOKIJUA NISHA KUJILIPUA KWA MZUNGU

Salma Jabu ‘Nisha’ DAR ES SALAAM: LICHA ya kuapa kwamba hataanika tena uhusiano wake, msanii wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’,  amejilipua kwa kumwanika mpenzi wake wa sasa ambaye ni Mzungu.

Awali, Nisha aliweka video kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram ikimuonyesha wakionyeshana vitendo vya kimahaba na mpenzi wake huyo huku akisindikiza na maneno kwamba imekuwa vigumu sana kuficha hisia kwa mtu anayempenda.

“Nimeshakuwa na wanaume weusi, Waarabu ila kote niliambulia usaliti na uongo wa mapenzi, niliwahi sikia Wazungu wana mapenzi ya kweli kuliko Waafrika… kujaribu si mbaya, mimi ni msafiri sijafika bado na Mwenyezi Mungu anajua kama hapa ndiyo mwisho wa safari yangu au inaendelea kikubwa nimeshampata na maneno sijali,” aliandika Nisha.Image result for salma jabu nisha NA MZUNGU WAKE

Baada ya mrembo huyo kuweka video hiyo Instagram, makaburi yalianza kufukuliwa ambapo katika kurasa za udaku waliweka picha ya Mzungu huyo akiwa na mwanamke ikidaiwa kuwa ni mke wake na Nisha amemchukua mume wa mtu.

Kutokana na suala hilo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Nisha ambapo mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo;

Risasi: Vipi Nisha, uliyemwanika mkiwa mnaoneshana mahaba mtandaoni ndiye shemeji yetu?

Nisha: Ndiyo, ni mpenzi wangu.

Risasi: Anaitwa nani na ni raia wa nchi gani?

Nisha: Jina siwezi kuliweka wazi, ni raia wa Italia.

Risasi: Kwa nini umeamua kuwa na Mzungu?

Nisha: Nimeamua kujaribu kwa Mzungu maana nilishakuwa na Waafrika na Wahindi lakini niliambulia maumivu.

Risasi: Inasemekana huyo ni mume wa mtu lakini?

Nisha: Walimwengu huwezi kuwakataza kuongea, kama wana ushahidi wa vyeti vyake vya ndoa waniletee.

Risasi: Kuna habari kwamba hii ni kiki maana una mpango wa kutoa muvi mpya uliyomshirikisha huyo Mzungu maana naye ni mwigizaji, hili likoje?

Nisha: Hii siyo kiki bali ni mpenzi wangu halisi, wamekuwa wakinisema kwamba nakuwa na wanaume wadogo lakini kwa sasa nimempata saizi yangu lakini cha kushangaza hata huyu wanamsema kwamba ni babu sijui hawa walimwengu wanataka nini/?

STORI: Gladness Mallya, Risasi Mchanganyiko

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment