The House of Favourite Newspapers

Nisha; Sarakasi Hizo Waachie Watoto

Salma Jabu ‘Nisha’

UKISEMA uzungumzie mion­goni mwa wasanii wa Bongo Movie warembo yaani ‘visu’ kwelikweli huwezi kuliacha jina la Nisha japo jina halisi alilopewa na wazazi wake ni Salma Jabu.

Nimeanza kumjua msanii huyu kitambo kidogo kipindi kile akipewa nafasi na Kampuni ya Ray na Johari (RJ) katika filamu yake ya kwanza kabisha kuwepo ya My Dream, ni mcheshi ukikutana naye na hata likija suala zima la kuigiza bi’dada huyu anaweza.

Salma Jabu ‘Nisha’

Kama umepata kubahatika kuzi­ona filamu zake za Simu Sikioni, Because of Facebook, Chumba cha Siri, Mchana wa Kiza, Bado Niko Hai, Pusi na Paku, Kiboko Kabisa, Zena na Betina, Hakuna Matata pamoja na Shida akiwa na Gabo Zi­gamba utaelewa namaanisha nini.

Huwa namkubali sana hasa ana­poigiza akichanganya vituko vyake hapa na pale. Hiyo imekuwa kama staili yake katika kuigiza, ucheshi na masihara yana­kuwa mengi lakini ujumbe unafika hicho ndicho kipaji alichoajaali­wa.

Katika filamu zake nyingi ame­kuwa akim­tumia King Majuto pamoja Hemed na kolabo yao hiyo huwa ni moto wa kuotea mbali kwani Nisha ana­kuwa Nisha kweli na Majuto anakuwa Majuto kweli.

Ukiachana na suala lake la filamu, katika maisha ya kawaida msanii huyu amekuwa na sarakasi nyingi za kimapenzi za hapa na pale ambazo nyingine kama zime­kuwa zikimshushia jina.

Aliwahi kuingia kwenye uhusiano na staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na kudaiwa kuwa ndiyo chanzo cha msanii huyo kuachana na mzazi mwenzake, Siwema Edson.

Nisha hakuishia hapo, baa­daye aliingia kwenye uhusiano na aliyekuwa mwanaume wa mwanamuziki Zuwena Mohamed ‘Shilole’ aliye­julikana kwa jina la Boy Caro na kuwa naye kwa muda mfupi kabla ya kutengana.

Haikuishia hapo, aliwahi kuhusishwa kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Barakah The Prince lakini napo hawakudumu kwa muda mrefu wakaachana na kuanzisha uhusiano na ‘kibenten’ aliyemtambulisha mwenyewe kwa jina la Minu.

Minu hakudumu sana na Nisha, aliachana naye na kuanzisha uhusiano na msanii mwingine, Snura Mushi.

Baada ya Snura ‘kumpora’ Minu mchumba wake, Nisha alitafuta pa kuegemea na kumbeba mzimamzima bwana wa staa mwenzake wa filamu, Jacqueline Wolper Massawe, Barnaba Shelu­kindo ‘Brown’.

Sipendi kuingilia sana huko japo inasemekana kwamba Nisha na Brown walishaanza kunyemeleana kitambo tangu jamaa huyo akiwa mikononi mwa Wolper me­kana kwamba, kufuatia uwepo wa mawasiliano ya siri kati ya Nisha na Brown, jamaa huyo alianza kuleteana vimbwanga vya kila kukicha na Wolper mwishowe wakaachana na kuingia rasmi kwa Nisha.

Kwa sasa imekuwa si kificho tena, ukiingia katika mitandao ya kijamii hususan Instagram, Nisha amekuwa akimuanika Brown na kumpa sifa kemkem, mbali na hilo amekuwa akiposti picha za mapozi ya kima­haba bila wasiwasi.

Kikubwa ninachotaka kukiweka sawa hapa, Nisha atambue kuwa ni staa mkubwa tu wa filamu, hayo ya kudaiwa kutoka na ma­bwana wa wasanii wenzake aangalie jinsi ya kuepukana nayo kwani sarakasi ana­zozifanya ni za kitoto.

Watch out!

 

Comments are closed.