The House of Favourite Newspapers

#NishusheDarLive: Roma, Darassa, Stamina, Blue na Snura Kuangusha Mistari Idd Mosi Dar Live

0
Darasa Mara ya mwisho kutinga Dar Live ilikuwa Mkesha wa Mwaka Mpya.

MACHO na masikio ya mashabiki wengi wa burudani kwa sasa yameelekezwa Sikukuu ya Idd Mosi katika kiwanja kimoja tu yaani Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar ambapo wakali kibao wataangusha mistari wakiongozwa na R.O.M.A Mkatoliki.

Itakuwaje?

Katika usiku huo, pazia la burudani litafunguliwa rasmi mapema kuanzia saa 2:00 asubuhi ambapo burudani ya watoto itatolewa chini ya kundi la sarakasi na kudensi la Wakali Dancers pamoja na Kundi la Muziki wa Asili la Makhirikhiri kutoka Tanzania.

Wakizungumza na Showbiz kwa nyakati, wakali hao watakaoongozwa na R.O.M.A Mkatoliki walisema kuwa siku hiyo itakuwa shoo ya kibabe kutoka kwa wakali wa kibabe katika jukwaa moja la kibabe Dar Live.

R.O.M.A Mkatoliki

“Kwa muda mrefu sijafanya shoo tangu nipate matatizo hapa kati. Mara ya mwisho nilifanya shoo Dar Live nikiwa na Darassa ilikuwa Usiku wa Michano (Mkesha wa Mwaka Mpya) na waliofika waliona na ambao hawakufika walisimuliwa. Safari hii nisingependa ikupite.

“Baada ya kupata matatizo ya kutekwa hapa kati, sasa nimepona na nipo fiti hivyo nguvu yote naihamishia Dar Live sikukuu hii ya Idd Mosi. Njooni kwa wingi kumshuhudia mchawi wao nikiwapagawisha na ngoma kibao kama vile Viva Roma Viva, K, Ivan, Kaa Tayari na nyingine kibao.”

Darassa

“Baada ya mwaka jana kuwadatisha na Muziki kwa mara ya kwanza Dar Live, safari hii nakwenda na ngoma nyingine tena ya Hasara Roho ambayo nayo ni amshaamsha.

Sina maneno mengi; ‘Dunia iweke tuzo za wachukiaji,

Bongo kuna watu wana vipaji,

Utarusha madongo kwenye maji,

Bora upige michongo utanipa midadi.’

Stamina

“Siku zote battle zangu jukwaa huwa linaongea. Michano hapa ndiyo nyumbani kwao, mashabiki wajiandae kumsikia na kumuona Stamina akiwa na ngoma kibao mpya ikiwemo Love Me na siku hiyo ni mperampera mwanzo mwisho hadi kuchee.”

Mr. Blue

“Wananiita Byser au mzee wa Baki Na Mimi! Pliz usikose Idd Mosi hii Dar Live kijana wenu nimewaandalia vitu kibwena! Nitaliamsha dude na ngoma zangu zote kali kama Pesa, Mboga Saba, Baki Na Mimi na nyingine kibao. Muhimu mashabiki mjitokeze kumuona Byser mpya najua mnajua muziki wangu jukwaani upoje. Haina kukata pumzi hiyo!”

Snura Akifanya yake ndani ya Dar Live

Snura

“Nina zawadi kibao za kuwapa mashabiki wangu Sikukuu ya Idd Mosi Dar Live. Mbali na kuwaimbia nitawaonesha live staili ya kucheza nyimbo zangu zote kuanzia Ushaharibu, Majanga, Chura, Najidabua, Shindu hadi wa sasa huu wa Nionee Wivu nilioimba na Yamoto Band.”

Zanzibar Stars

Mmoja wa wanaounda Kundi la Zanzibar Stars, Mosi Suleiman alisema;

“Zanzibar Stars itazaliwa upyaaa Idd Mosi Dar Live. Wapenda Muziki wa Mwambao hii si ya kukosa kwani tumewaandalia vibao vipya kabisa kutoka kwa wakali wengi wakiwemo Bi. Mwanahawa, Jokha Kassim, Mosi Suleiman na Zubeda Mlamali.”

Bambo

“Nitaliamsha kuanzia asubuhi mpaka mida ya jogoo akitoka bandani. Mkongwe niliyebaki katika uchekeshaji Bongo nitakuwepo kufanya yangu kwa watoto na wakubwa wote watak-aofika Sikukuu ya Idd Mosi Dar Live.”

Mto-nyo je?

Mratibu na Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo aliweka wazi kuwa licha ya uwepo wa wakali wengi, kiingilio kwa siku hiyo upande wa shoo ya kibabe itaka-yoanza saa 2:00 usiku kitakuwa kiduchu tu yaani shilingi 7,000 huku watoto ikiwa shilingi 3,000 tu na bonasi ndani yake ya kuteleza bure, kubembea bure, kupanda ndege bure, kuogelea bure na vingine vingi bureee.

Leave A Reply